Kwa mujibu wa staa huyo ambaye kwa sasa anaminya kimapenzi na
mtangazaji wa DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’, msikiti huo utakuwa
kumbukumbu yake kwa watakaoutumia kama sehemu ya kurudisha kwa…
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Na Sifael Paul Global Publishers
SIKU chache baada ya kuwachefua Waislamu wenzake kwa kutimba kwenye
Maulid na kuomba dua akiwa amevaa hereni na mkufu, msanii wa Bongo Fleva
mpenda totoz, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ametangaza kujenga
msikiti jijini Dar es Salaam, kwani ni jambo alilolipanga kwa muda
mrefu.
Kwa mujibu wa staa huyo ambaye kwa sasa anaminya kimapenzi na
mtangazaji wa DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’, msikiti huo utakuwa
kumbukumbu yake kwa watakaoutumia kama sehemu ya kurudisha kwa jamii
inayompa sapoti kubwa.
Diamond ambaye amemjengea mama yake, Sanura
Kassim ‘Sandra’ nyumba ambayo hadi sasa imegharimu Sh. milioni 260
alifunguka: “Ninajitahidi sana kununua viwanja au vinyumba vidogovidogo
maeneo tofauti. Nipo kwenye plan (mpango) ya kujenga msikiti japo
sijapanga sehemu hasa hadi nipate eneo la kutosha.
“Nataka iwe kumbukumbu ili hata kesho na keshokutwa nikifa, vizazi vijavyo wawe wanaswali kwenye msikiti uliojengwa na Diamond.
“Kwa kufanya hivyo itanipa baraka kubwa sana na soon tu nina imani mwenyezi Mungu atanisaidia nijenge huo msikiti.”