Papa mpya Francis Vatican
....akiwa pungia mkono waumini waliofika eneo hilo wakati wa kutangazwa kwake
Kazi ya kuchaguwa wasaidizi…
Papa Francis I (katikati) akiwa na Kardinali Santos Abril wa Hispania (kushoto) na Kardinali Agostino Vallini ambaye pia ni Kasisi Mkuu (Vicar General) wa Roma (kulia) wakiupungia umati leo asubuhi.
Papa Francis I akihutubia kwa mara ya kwanza baada ya kuchaguliwa.
Siku yake ya kwanza ofisini kama Papa mtakatifu wa kanisa Katoliki,
Papa Francis 1 tayari anaanza kazi. Papa anatarajiwa kuwateua
wafanyakazi wakuu watakaohudumu katika Vatican chini ya uongozi wake.
Ameanza siku yake kwa maombi ya kibinafsi katika hekalu ya mtakatifu
Maria Maggiore mjini Rome. Baadaye Papa atafanya misa ya sherehe katika
kanisa la Sistine.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa uteuzi atakaofanya Papa Francis,
utatizamiwa kama ishara ya mageuzi katika uongozi uliozongwa na kashfa
nyingi na pia utaonyesha mwelekeo anaonuia kuchukua kwa kanisa hilo.
Baadaye wikendi ijayo, Papa mpya anatarajiwa kukutana na vyombo vya habari vya dunia katika mkutano maalum.
Na Jumapili, ataongoza misa yake ya kwanza kama papa. Hata hivyo yeye
mwenyewe atatawazwa rasmi kuwa Papa Francis 1, siku ya Jumanne.
Chanzo: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment