Uchaguzi wa kuwachagua maseneta nchini Liberia.
Idadi ndogo ya wapiga kura imeripotiwa kwenye kura ya kuwachagua maseneta nchini Liberia.
Kura
hiyo ilikuwa imeahirishwa mara mbili kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa
ebola na huenda hofu ya ugojwa huo iliosababisha watu kukosa kufika kwa
vituo vya kupigia kura.Wapiga kura walishauriwa kusimama umbali wa mita moja kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine walipokuwa wakipanga milolongo kupiga kura baada ya viwango vyao vya joto kuchukuliwa na maafisa wa afya.
Polisi wanasema kuwa mahema yalichomwa na wafanyikazi wakafukuzwa na megenge ya vijana.
Jamii kwenye sehemu zingine za magharibi mwa afrika zilipinga jitihada za kukabiliana na ugonjwa huo zikihofia kuwa huenda zikapata maambukizi kutoka kwa wafanyikazi wa kutoa huduma za afya. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Na BBC
No comments:
Post a Comment