Sunday, December 21, 2014

U.S.A YAITAKA KOREA KASKAZINI KUILIPA SONY

Wakuu wa kampuni ya filamu ya Sony Pictures.Marekani imeitaka Korea Kazkazini kuilipa kampuni hiyo kwa hasara iliopata baada ya madai ya kuhusika na uhalifu wa mtandao dhidi yake.
 
Marekani imezitaka China na nchi zingine kuthibitisha kuwa Korea Kaskazini ilihusika na uhalifu wa mtandao dhidi ya kampuni ya Sony Pictures.
Marekani inasema kuwa Korea Kaskazini ni lazima ikiri kuwa ilihusika na iilipe Kampuni ya Sony kutokana na hasara ambayo imepata
Korea Kaskazini imeyataja madai hayo ya Marekani kuwa ya uongo.
Wataalamu wanasema kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuwa Korea Kaskazini ilihusika.
Lakini mwandishi wa BBC nchini Korea Kusini anasema kuwa kampuni ya Sony Pictures nchini Marekani na wakuu wake nchini Japan watahitajika kuamua iwapo wataonyesha filamu ya uchesi yenye utata ya rais wa Korea Kazkazini Kim Jong-un. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Na BBC

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...