Kocha Hans Van Der Pluijm akiwa na Boniface Mkwasa katika moja ya mechi za Yanga Uwanja wa Taifa.
BAADA ya kupewa mkataba wa mwaka moja na nusu kukinoa kikosi cha
Yanga kocha Hans van der Pluijm ameomba siku saba kuibadili timu hiyo.
Pluijm alisema atahakikisha anatoa mbinu zake zote alizokuwa nazo za
ukocha ili aweze kuipa mafanikio timu hiyo msimu huu ikiwemo kutwaa
ubingwa wa Tanzania bara.
Pluijm aliyetua Yanga kwa mara ya pili akichukua nafasi ya Mbrazil
Marcio Maximo alisema kwa kuanza atatumia siku saba kwa ajili ya
kubadilisha mfumo na kasi ya wachezaji ili waweze kushinda mchezo wao wa
Ligi Kuu dhidi ya mabingwa watetezi Azam FC utakaopigwa Uwanja wa Taifa
Desemba 28.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
“Najisikia furaha sana kuwa kocha wa Yanga kwa mara ya pili ni
heshima kubwa waliyonipa kwasababu hii ni timu yenye uwezo mkubwa wa
kuajiri kocha kutoka bara lolote lakini imeamua kunirudisha mimi
kulitambua hilo nimedhamiria kutoa kila nilicho nacho kiufundi kwa ajili
ya kuijenga Yanga mpya, alisema Pluijm.
Pluijm alisema anaamini kazi yake haitakuwa ngumu kutokana na ubora
wa wachezaji wanaounda kikosi hicho ambao wengi wao walikuwepo kabla
hajaondoka nchini kujiunga na klabu ya Al Shaula ya Saudi Arabia hivyo
amewataka kuwa na utulivu huku wakisubiri kuanza kuona kazi yake Desemba
26.
“Nimeiona Yanga ikicheza msimu huu ni kweli imeshuka kidogo lakini
haitakuwa kazi kubwa kuirudisha katika kiwango chake ndiyo sababu
nikatoa siku saba nikiamini haitakuwa kazi kuirudisha katika kiwango cha
awali kutokana na mbinu zangu nitakazozitumia,” amesema Pluijm.
Pluijm alisema atakapofanikiwa kuirudisha timu hiyo kwenye kiwango
chake kitu ambacho kitafuatia ni kupigania ubingwa wa kwani ameona
hakuna tofauti kubwa ya pointi kati yao na timu inayoongoza ligi Mtibwa
Sugar.
“Nimeona kuna tofauti ya pointi mbili kati ya Yanga na Mtibwa Sugar
ni kitu kizuri kwangu kwasababu kazi yetu kubwa itakuwa kuhakikisha
tunashinda kila mchezo wetu ili kukimbizana na wanaoongoza ligi Mtibwa
Sugar.
Pluijm amewataka mashabiki wa Yanga kusahau machungu ya kufungwa na
watani zao Simba Jumamosi iliyopita kwenye pamla Nani Mtani Jmebe 2 na
kuendelea kuwapa sapoti wachezaji wao ili waweze kufanya vizuri katika
ligi inayotarajia kuendelea Desemba 26 mwaka huu. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
No comments:
Post a Comment