Sunday, December 21, 2014

SERIKALI YAONYA DAFTARI LA WAPIGAKURA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Mh. Willium Lukuvi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) William Lukuvi, ameonesha kutoridhishwa na utaratibu mbovu unaotumika kuandikisha wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura, kutokana na kuwa na mianya inayoweza kuingiza wasio raia wa Tanzania.
Lukuvi aliyasema hayo jana, wakati alipotembelea kituo cha Bunju A kuangalia uandikishwaji wa wananchi kwa kutumia teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration (BVR).
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Bunju A ambayo ipo jimbo la uchaguzi Kawe ni miongoni mwa maeneo yaliyo katika majaribio ya mfumo huo. Maeneo mengine ni Mlele (Katavi) naKilombero mkoani Morogoro. Alisema utaratibu unaotumika katika uandikishwaji katika daftari hilo, hauridhishi kutokana na wananchi kutoa taarifa zao bila kuwa na vielelezo vyovyote vinavyothibitisha uraia wao, jambo linaloweza kusababisha matatizo.
“Wekeni hata watu watakaoweza kuthibitisha taarifa za waandikishwaji, kwa sababu wanaweza wakajitokeza watu ambao sio raia na utakapowapa kitambulisho cha kupigia kura huwezi kumwambia sio raia, kuweni makini sana,” alisema Lukuvi. Akizungumza na wananchi waliofika kujiandikisha katika kituo hicho, aliwataka kuhakikisha wote wanaojiandikisha wawe wakazi wa eneo hilo ili kuondoa usumbufu baadaye wakati wa kupiga kura.
“Kama kuna wakazi wa Manzese na eneo ambalo sio hili tafadhalini sana ondokeni, kwa sababu itakuja kuwaletea usumbufu wakati uandikishaji kamili ukianza na pia inaweza kusababisha ukakamatwa kwa kuwa utakuwa umetoa taarifa za uongo,” alisema.
Aidha, Lukuvi alimuagiza Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Uchaguzi( NEC), Julius Mallaba kuhakikisha wanasimamia mfumo huo vizuri ili waweze kuaminika kwani uandikishwaji huo utakapokwenda vibaya serikali ndiyo italaumiwa. Alisema serikali imetekeleza kile ambacho NEC ilikiomba na hivyo ni jukumu lao kuhakikisha uandikishwaji huo unakwenda vizuri.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Vitambulisho hivyo imeelezwa vitatumika kwenye kura za maoni pamoja na Uchaguzi Mkuu. Mbali na wakazi wa maeneo yaliyofanyiwa majaribio ya uandikishaji kwa kutumia mfumo huo, Lukuvi alisema wakati kazi ya uandikishwaji itakapoanza mwakani ni lazima irudiwe upya hata katika maeneo hayo ili kuhakikisha kila mmoja mwenye vigezo anapata kadi ya mpiga kura na pia kujiridhisha na vigezo vya waandikishwaji.
Aidha, Lukuvi alionya kuhusu kutegemea mawakala wa vyama, ambapo alisema haifai kuwategemea kutokana na kila mmoja anaweza kuwa na maslahi yake binafsi au ya chama chake. “Sio kwamba msiwatumie kabisa hapana wanaweza wakawepo na watu wengine pia wakawepo.
Na kwa wale wenye vitambulisho vya taifa ni vizuri mkawa na vifaa vitakavyoweza kusoma taarifa zao ili kurahisisha zoezi na taarifa zisitofautiane. “Serikali imewawezesha kutekeleza teknolojia mliyoitaka, hivyo ni lazima muisimamie vizuri. Lakini nasisitiza wekeni utaratibu mzuri, inaonekana waandikishwaji hawajapewa taarifa zozote,” alisema.
Hata hivyo, Mallaba alisema, changamoto kubwa iliyopo ni uchache wa vifaa vilivyopo jambo linalochangia uandikishwaji kwenda taratibu tofauti na vile walivyokuwa wamepanga. “Tunajitahidi kutatua changamoto zilizopo lakini pia ufinyu wa vitendea kazi unachangia, tulikuwa tumepanga zitumike dakika nne katika kuandikisha mtu mmoja lakini sasa inaenda mpaka dakika sita,” alisema.
Wakizungumza na gazeti hili, baadhi ya wananchi waliofika kujiandikisha katika kituo hicho cha Bunju A, walisema utaratibu unaotumika katika uandikishaji umekuwa ni mbovu tofauti na miaka iliyopita. Mariagoreth Joseph alidai, utaratibu uliopo hauridhishi kwani tangu alipokwenda kituoni hapo juzi na kuandikisha jina hakuweza kupiga picha hadi jana, jambo alilolalamika kuwa wanapoteza muda mwingi.
“Nimekuja jana (juzi) nikaishia kuandika jina tu, hata picha sijapiga na leo (jana) nimekuja tangu asubuhi mpaka sasa hakuna kinachoendelea muandikishaji yupo mmoja tu na huyo huyo wakati mwingine anaenda kuwapiga watu picha,” alisema. Naye Halima Mbonde alidai, wameacha shughuli zao za kujiingizia kipato lakini uandikishwaji huo umetawaliwa na vurugu.
“Hawa wenyewe wanatuonesha kuwa vitambulisho hivi havina umuhimu, kwa sababu hata wenyewe hawana umakini na sisi tutachoka tutaacha kujiandikisha, wengine tuna watoto kama hivi ni taabu tuko hapa tangu asubuhi,” alisema.
Nchi zinazotumia mfumo wa BVR na mwaka ulioanza kwenye mabano ni Nigeria (2007), Liberia (2005), Ghana (2009), Guinea na Mali (2005), Uganda na Zambia (2008), Kenya (2013), Afrika Kusini, Zanzibar (2009) na Namibia (2014).
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Na Habari Leo 

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...