Rais Jakaya Kikwete akihutubira wazee wa mkoa wa Dar es Salaam kwenye
ukumbi wa Diamond Jubilee jijini hapa.
Rais Jakaya Kikwete amesema fedha
zilizochotwa katika Akaunti ya Tegeta Escrow hazikuwa zinafikia Sh306
bilioni, bali ni Sh202 bilioni na zilikuwa mali ya Kampuni ya Kufua
Umeme ya IPTL.
Akijibu swali alilojiuliza mwenyewe katika hotuba
yake ya zaidi ya saa mbili kuwa: “Fedha hizi mwenyewe nani, umma au
IPTL?” Rais Kikwete alisema kumekuwapo na maneno mengi, kila mtu anasema
yake na wenzangu Wakwere tunasema ‘tunazoza sana’ akimaanisha waongea
sana.
Alisema, “Kimsingi fedha hizi ni za IPTL, katika
swali pesa za nani, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
alipoulizwa na Kamati ya Bunge alisema humu yawezekana zipo za umma pia
zipo za IPTL.
“Nilipomuuliza maana, akasema zamani walikuwa
wanalipa moja kwa moja kwa Tanesco lakini baada ya mzozo walikubaliana
kwanza waziweke Benki Kuu ya Tanzania (BoT).”
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Akielezea maana ya escrow, alisema, “Ni tofauti
kidogo na akaunti zetu tatu tulizozizoea, ni akaunti maalumu ya kazi
maalumu na kazi hiyo maalumu ikiisha inafungwa. Inasimamia na wakala na
wakala pia ana jukumu la kumlipa mwenye fedha wakati ukifika.”
Ukumbi uliojaa wazee na wasio wazee wakimsikiliza
kwa umakini ulikuwa umetulia kimya alipoanza kuzungumzia sakata hilo,
akisema akaunti hiyo ilifunguliwa BoT kwa ajili ya kuweka fedha za tozo
ya uwekezaji, ili kutoa nafasi kwa pande mbili kushughulikia tofauti
zao.
“Kama mgogoro ungetatuliwa na madai ya Tanesco
yakakubaliwa na tozo kupunguzwa, katika kiasi kilichopunguzwa kuna pesa
za Tanesco ambazo lazima zirudi, bahati mbaya miaka saba baadaye hilo
(la maelewano) halikuwa limefanyika.”
“Kama katika fedha hizo ipo kodi ya Serikali na
kwa mujibu CAG kulikuwa na Kodi ya Ongezeko la Thamani (Vat) ambayo
haikulipwa, IPTL hawakuilipa na uthamini ulikuwa zaidi ya Sh21.7 bilioni
na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imepeleka madai yake kwa PAP,”
alisema Rais Kikwete.
Aliongeza: “CAG aliwaelekeza Tanesco kuacha
kuhesabu fedha walizolipa kwenye Akaunti ya Escrow kama yao, pesa
hazikufikia sifa kuhesabika kama mali ya Tanesco. Mahakama Kuu ya
Tanzania ilifanya uamuzi katika shauri la maombi ya VIP, kusimamisha
mchakato wa ufilisi wa IPTL na Mahakama ikakubali.”
Alisema Wizara ya Nishati na Madini ilimwandikia
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (wakati huo), Jaji Frederick Werema kuomba
ushauri na aliwashauri; “walipeni, uamuzi uko sawa na hauna matatizo na
BoT waliuliza maswali hayohayo na majibu yakawa yaleyale.”
Alisema: “Kwa kuzingatia ushauri huo akaunti
ikafungwa na pesa kukabidhiwa PAP. Mjadala ukaendelea bungeni na kwenye
mablogu. Hata Tanesco ilipewa ushauri huohuo, uamuzi ule umetiliwa shaka
na kuonekana haukuwa sahihi na umeitia hasara nchi. Ukaibua hisia na ni
kwa sababu nzuri tu kwamba si bure na iko namna kama ya rushwa na watu
kunufaika binafsi. Mara kuna watu wamekwenda benki na kubeba pesa
viroba, kwenye sandarusi, lumbesa na mengineyo.”
Alisema, “Nilipokutana na Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, alisema hakukosea katika ushauri wake na wala Mahakama
haikufanya makosa na huo ndiyo ulikuwa msimamo wake na mpaka sasa bado
anaamini hivyo kuwa fedha si mali ya umma.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
“Kuhusu hasara iliyopatikana alisema hakuna
hasara yoyote iliyopatikana kwa sababu fedha ililipwa kwa mtu halali.
Kwa upande wa kodi ya Serikali ambazo hazikulipwa, AG alipoulizwa
alisema hakuna kodi iliyochelewa kulipwa. Yamesemwa mengi na bado
hatujamaliza kuyasoma, rushwa ni kosa la jinai. Nilielekeza taarifa
walizozipata wazipeleke Takukuru. Nimeambiwa wanaendelea na mchakato
wao.
No comments:
Post a Comment