Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi
(CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amesema upepo wa kisiasa unakivumia
vizuri chama chake na ana matumaini Uchaguzi Mkuu ujao kitapata viti 18
vya uwakilishi katika ngome ya CCM Unguja.
Hivi sasa CUF inashikilia majimbo manne ya Unguja
kati ya 32 na kwa muda wote ngome yake imekuwa ni Pemba kinakoshikilia
majimbo yote 18.
Akihutubia mkutano wa hadhara baada ya kuzindua
miradi ya maendeleo katika Jimbo la Magogoni, Wilaya ya Magharibi
Unguja, Maalim Seif alisema suala la Katiba Mpya na ufisadi uliokithiri
vitaipa wakati mgumu CCM, hasa upande wa Zanzibar.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

“Hivi sasa Unguja tuna majimbo manne, lakini
katika uchaguzi mkuu ujao tutapata si chini ya 18 ukijumuisha na 18 ya
Pemba, CUF tutaunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa tukiwa na nguvu ya
uamuzi,” alisema Maalim Seif.
Maalim Seif alisema CUF inaweza kupata majimbo
zaidi ya hayo Unguja, lakini dhamira yake ni kuwa na Serikali ya Umoja
wa Kitaifa, hivyo si busara viti vyote vya uwakilishi na ubunge vikawa
vinashikiliwa na chama hicho.
Maalim Seif, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa
Rais wa Zanzibar kutokana na maridhiano yaliyounda Serikali ya Umoja wa
Kitaifa (SUK), alisema CCM wanajua hali ni mbaya upande wa Zanzibar na
hivi sasa baadhi ya viongozi wake wamekuwa wakisikika wakisema, “hatutoi
Serikali”.
“Silaha yetu ni mshikamano wetu tukishikamana,
hakuna wa kutuzuia kuongoza Serikali ya Umoja wa Kitaifa, wanaoamua ni
wananchi si Maalim Seif, si Shein wala si Balozi Seif Ali Iddi,” alisema
Maalim Seif.
Alisema hakuna Mzanzibari aliye tayari kuipigia
kura ya ndiyo Katiba Inayopendekezwa kwa sababu inainyonga Zanzibar,
hivyo ni wazi suala hilo lina ufisadi.
Kuhusu ongezeko la matukio ya uhalifu, alisema yatadhibitiwa kwa jamii kuunga mkono dhana ya ulinzi shirikishi.
Alisema Jeshi la Polisi peke yake haliwezi
kumaliza matukio ya uhalifu, ikiwamo ujambazi, watumiaji na wauzaji wa
dawa za kulevya na watu wanaofanya udhalilishaji watoto na wanawake,
lakini jamii kupitia mpango wa ulinzi shirikishi ndio watakaoyamaliza.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Na Mwananchi

No comments:
Post a Comment