Tuesday, December 23, 2014

PLUIJM AWALILIA KASEJA NA KIIZA

Kocha wa Yanga, Hans Van Pluijm akiteta jambo na wachezaji wake, siku za hizi karibuni. Picha na maktaba 

Kocha wa Yanga, Hans Van Pluijm amesikitishwa na kitendo cha kuondoka kwa nyota wake Juma Kaseja, Hamisi Kiiza na Didier Kavumbagu, lakini akawataka wachezaji wake wasahau yaliyopita na waangalie yajayo.
Pluijm amechukua mikoba ya Marcio Maximo aliyetupiwa virago baada ya Yanga kufungwa na Simba 2-0 katika mchezo wa Nani Mtani Jembe kama ilivyokuwa mwaka jana alipoinoa timu hiyo kwa mara ya kwanza baada ya Ernie Brandts kutimuliwa kutokana na timu hiyo kunyukwa 3-1 na Simba.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Pluijm alisema Kaseja alikuwa nahodha, lakini sasa hayupo kutokana na tofauti zake na viongozi.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
 
“Nimefika hapa, hayupo Juma, hayupo Kavumbagu, hayupo Kiiza. Kibinadamu kama watu uliozoea kufanya nao kazi ukisikia uongozi umewaondoa inauma. Sitaki kujua sababu, wala sitaki kuingilia masuala yao, lakini roho inaniuma, ni kama mwanafamilia akifariki mtalia sana, roho zitauma, mtasikitika, lakini mwishowe maisha ni lazima yaendelee,” alisema Pluijm.
“Nawaheshimu wachezaji waliopo, nimeshaongea nao kikubwa nimewaambia wasahau yaliyopita. Wasisikitike kuondoka kwa wenzao, wasisikitike kuondoka kwa kocha, yaliyopita yamepita sasa tuanze maisha mapya, tukiwa na lengo moja la kuifanya Yanga iwe juu.
“Niliondoka na kuiacha Yanga katika nafasi nzuri na sasa nimerudi nyumbani. Ushirikiano baina ya wachezaji, viongozi na mashabiki ndiyo utaifanya Yanga ipate mafanikio zaidi kwenye ligi na mashindano ya kimataifa.
“Najua ligi msimu huu ni ngumu zaidi na kila timu inahitaji mafanikio, Yanga iko kwenye nafasi ya pili na bahati nzuri jana (juzi) nimekaa na wachezaji na kuzungumza nao kuwa umoja kati yetu ndiyo utatusaidia kutwaa ubingwa.”
Mdachi huyo aliongeza kusema: “Kikubwa nilichowataka ni kujitambua, Yanga ni klabu kubwa, kama mchezaji anapata nafasi, basi ajue jukumu lake. Mkakati wangu ni kuhakikisha Yanga inacheza soka la kuvutia na mpangilio mzuri. Najua wote ni binadamu na kuna makosa ya kibinadamu, lakini ninawataka kila mmoja acheze kiushindani na morali ya hali ya juu.
“Kazi yangu kama kocha ni kuwajengea wachezaji morali, naipenda timu yangu. Tunatakiwa tushirikiane, viongozi watimize wajibu wao, mimi kama kocha nitimize wajibu wangu na wachezaji pia watimize wajibu wao wacheze kwa kutumia akili na soka la kuvutia”.
Hata hivyo, Pluijm aligoma kuweka wazi mkakati wake atakaoutumia kuhakikisha Yanga inachukua taji la Ligi Kuu kwa kile alichodai kuwa fomesheni siyo inayofanya kushinda mchezo.
“Ushirikiano na kujituma ndiyo kunakowezesha kushinda mchezo, sina hofu na wachezaji, nina hofu na mbinu zangu nitakazowapa kama watazielewa na kuzitekeleza. Kuna wachezaji wapya ambao siwafahamu, miezi minne ni michache kusema naweza kuiweka Yanga kwenye kiwango cha juu, itawezekana kukiwa na ushirikiano wa kutosha,” alisema Pluijm.
Wakati huohuo, sekretarieti mpya ya Yanga ikiongozwa na katibu mkuu, Dk Jonas Tiboroha leo inaanza kazi rasmi.
 Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro Sekretarieti hiyo itaanza kazi rasmi leo na kesho itajitambulisha kwa wanahabari.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...