Kampuni za Pan Africa Power
Solution Tanzania Limited (PAP) na Independent Power Tanzania Ltd
(IPTL), zimewasilisha maombi ya kutaka Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya
Mapato (TRA) akamatwe kwa kukiuka amri ya Bodi ya Rufaa za Kodi (TRAB)
kwa kufuta Hati za Malipo ya Kodi za Mauzo ya Hisa (Capital Gain
Certificate).
Kampuni hizo mbili, ambazo ziko kwenye mgogoro wa
umiliki, ndizo zinahusika kwenye sakata la uchotwaji wa Sh306 bilioni
kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow iliyofunguliwa kuhifadhi fedha za malipo
ya tozo ya kuuza umeme unaofuliwa na IPTL, kwa Shirika la Umeme
(Tanesco), wakati wa kusubiri uamuzi wa mahakama katika kesi ya kupinga
tozo hilo.
PAP, ambayo inadai imenunua hisa zote za IPTL,
ndiyo iliyolipwa fedha zote zilizokuwa kwenye akaunti hiyo na kuamsha
mjadala mkubwa bungeni ulioisha kwa Bunge kufikia uamuzi wa
kuwawajibisha kisheria wote waliohusika, wakiwemo mawaziri. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza
kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Lakini uamuzi huo wa Bunge haukuwa tamati la
sakata hilo baada ya kampuni hizo mbili kukata rufaa TRAB dhidi ya
Kamishna wa TRA na Msajili wa Kampuni na Leseni (Brela) zikipinga
kusudio la kufuta hati hizo.
Jana kampuni hizo mbili ziliwasilisha maombi ya
hati ya kutaka Kamishna Mkuu wa TRA akamatwe, zikidai kuwa amepuuza amri
hiyo iliyomzuia kutekeleza azma yake ya kufuta Hati za Malipo ya Kodi
ya Mauzo ya Hisa.
Katika maombi hayo walalamikaji hao wanadai kuwa
licha ya TRAB kutoa zuio hilo Novemba 26, 2014, Kamishna Mkuu wa TRA,
ambaye ni mlalamikiwa wa kwanza, alitoa amri ya kuziondoa hati hizo siku
iliyofuata, yaani Novemba 27, 2014, bila kujali amri hiyo.
Walalamikaji hao pia wanaiomba TRAB, baada ya
kumkamata Kamishna Mkuu wa TRA, itoe amri afungwe kwa kudharau amri
halali iliyotolewa na bodi na pia imwamuru akidhi matakwa ya amri ya
TRAB ya Novemba 26.
Pia walalamikaji hao wanaiomba TRAB imwamuru
mlalamikiwa huyo, kulipa gharama za uendeshaji wa shauri hilo pamoja na
amri nyingine ambazo itaona kuwa zinafaa.
Maombi hayo ya PAP na IPTL ya hati ya kumkamata na
kuamuru Kamishna Mkuu wa TRA afungwe yamepangwa kusikilizwa leo na
Katibu wa TRAB, Respicius Mwijage.
Hati ya kiapo inayounga mkono maombi hayo inaeleza
kuwa mlalamikiwa, akiwa ni raia wa Tanzania, siyo tu kwamba alipaswa
kuwa mtiifu kwa mamlaka ya bodi hiyo, bali pia alipaswa kutekeleza
sheria za nchi ambazo bodi hiyo ni sehemu yake.
Hati hiyo ya kiapo ya mkurugenzi wa operesheni wa
IPTL, Parthiban Chandrasakaran, inaeleza kuwa kwa kitendo hicho cha
kutotii amri ya bodi hiyo, mlalamikiwa amepoteza sifa ya kuwa mtumishi
wa umma katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pia inaelea kuwa kama bodi hiyo isipotumia mamlaka
yake kukubali maombi hayo ya kutoa amri inayoombwa, basi walalamikaji
watapata hasara isiyoweza kufidiwa.
Inafafanua hasara hizo kuwa ni pamoja na kodi nyingine ambazo tayari PAP wamelipa TRA kwa ajili ya kuendesha biashara.
Pia hati hiyo ya kiapo inafafanua kuwa kuondolewa
kwa hati hizo kutahatarisha biashara ya walalamikaji ambayo wamekuwa
wakiiendesha tangu walipota hati hizo.
Inaendelea kueleza kuwa kwa kuwa walalamikaji wako
katika hatari ya kuvunja mkataba na Shirika la Umeme (Tanesco), na
wadau wengine, jambo hilo litasabaisha vita ya kimahakama na hivyo
kulipa fidia zisizo za msingi.
Hati hizo namba 004965600 na 0049657 zilitolewa na
TRA Desemba 23, 2013, kwa ajili ya uuzaji wa hisa baina ya kampuni ya
Mechmar Corporation (Malaysia) Berhard iliyokuwa ikimiliki asilimia 70
ya hisa za IPTL na Piper Links Investment Limited na kati ya Piper Link
na PAP.
Hata hivyo baadaye, Novemba 19, 2014 TRA ilitoa
taarifa ya siku sita kwa Brela ikionyesha kusudio la kuziondoa hati hizo
kwa madai kuwa mkataba wa madai ya mauzo ya hisa hizo ulikuwa ni
mkataba wa makubaliano ya uongo.
Wakati Huohuo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
amesema kitendo cha kushindwa kuwachukulia hatua wanaotuhumiwa kuchota
Sh306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow hadi sasa, ni ishara ya
kuwa na Serikali dhaifu.
Mbowe, ambaye ni kiongozi wa Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni, alisema viongozi waliotuhumiwa kwenye kashfa hiyo
walitakiwa wawekwe kando kabla ya hatua zaidi.
“Leo (jana) ni siku ya tano na Rais Kikwete
ameshindwa kutoa uamuzi wowote. Hii inaonyesha jinsi tulivyo na Serikali
dhaifu,” alisema Mbowe wakati akihutubia mkutano wa kampeni za Uchaguzi
wa Serikali za Mitaa kwenye Kata ya Vijibweni, Kigamboni.
“Hadi leo Waziri wa Ardhi, Profesa Anna Tibaijuka
bado yupo ofisini na anasaini nyaraka mbalimbali za viwanja. Inakuwaje
hadi leo wezi bado wapo ofisini?”
, kwanini wanalindwa?” alihoji.
“Wanapewa muda wa kukaa ofisini kujipanga ili hata
Rais Kikwete atakapochukua uamuzi, wawe wamejipanga na kuchukua kidogo
kilichokuwepo.”
Mbowe alisema sakata la Escrow lilitikisa nchi na
kwamba kitendo cha watuhumiwa kutochukuliwa hatua hadi leo tafsiri yake
ni kwamba viongozi wa Serikali wanalindana. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza
kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Na Mwananchi
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment