Rais Robert Mugabe awalaumu baadhi ya wapinzani
wake ndani ya chama cha ZANU PF kwa kupanga kumuondoa mamlakani.
Rais
wa Zimbabwe Robert Mugabe amelaumu baadhi ya watu ndani ya chama chake
tawala cha ZANU-PF kwamba wanapanga kumng'oa madarakani.
Akizungumza
katika kongamano la chama hicho, Mugabe amesema amebaini kuwepo
majaribio ya kuwahonga wajumbe kumpinga kama kiongozi, lakini
akasisitiza wajumbe hawawezi kupokea hongo. Mugabe ameahidi
kupambana na rushwa ndani ya chama na kukabiliana na maafisa wa chama
hicho ambao kazi yao ni kutoa hongo na kupokea rushwa.
Wanachama wengi wa chama hicho wangali ni wafuasi sugu wa Rais Mugabe
Hasira ya Mugabe ilionekana
kufuatia madai ya njama ya kutaka kumuua yanayodaiwa kuandaliwa na
naibu wake Joyce Mujuru. Hata hivyo Mujuru alikanusha madai hayo ambayo
yamekuwa yakimuandamana.Mugabe alisema kutokuwepo kwa Bi Mujuru kwenye mkutano huo wa chama kunaonyesha kuwa anaogopa. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza
kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz Kadhalika Mugabe amesema Mujuru ni mwizi anayepanga kumuondoa mamlakani kwa kushirikiana na maafisa wengine wa chama.
Maelfu ya wajumbe wa chama walihudhuria kongamano hilo mjini Harare
Chama tawala cha Zimbabwe
kinakumbwa na vita vya ndani kwa ndani kuhusiana na nani atarithi nafasi
ya Mugabe ambaye ana miaka 91 na ambaye ameongoza tangu uhuru wa taifa
hilo.Hata hivyo amekanusha madai ya kwamba anataka kujiuzuru na kusema kuwa huo ni upuuzi. Hivi
karibuni afisa mwingine mkuu wa chama tawala, Robert Gumbo aliiambia
BBC kwamba Mugabe mwenye umri wa miaka 90 amegeuza chama tawala na
kukifanya kama mali yake binafsi.
Bi Joyce Mujuru amedaiwa kupanga njama ya kumuua Mugabe ili achukue mamlaka kutokla kwake. Gumbo alisema lengo kuu la Mugabe ilikuwa kuendeleza uongozi wa chama kwa niaba ya mke wake Grace.Bi
Mujuru ambaye amekanusha madai hayo alionekana kama mtu ambaye
anechukua usukani wa chama kutoka kwa Mugabe ambaye walipigania naye
uhuru wa nchi hiyo kutoka mikononi mwa watwala wazungu. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza
kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz Na BBC
No comments:
Post a Comment