MKAZI wa kijiji cha Chibwechangula –Behelo katika wilaya ya Mpwapwa
mkoani Dodoma, Ruth Matonya (26) amejifungua mtoto wa ajabu ambaye nusu
ya sura yake inafanana na binadamu na nusu ikifanana na chura.
Mtoto huyo alizaliwa Desemba 2, mwaka huu katika Kituo cha Afya cha
Mtakatifu Luka kinachomilikiwa na Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya
Mpwapwa. Alifariki dunia muda mfupi baada ya kuzaliwa.
Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Dk Edwin Kihura mara baada ya mama huyo kufika katika kituo hicho cha afya alikuwa na uchungu ambao haukuwa na kikomo, lakini alishindwa kujifungua kwa njia ya kawaida licha ya njia ya uzazi kufunguka.
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Alisema kutokana na hali hiyo iliwalazimu kumfanyia upasuaji mama
huyo kwa lengo la kuokoa maisha yake na mtoto. Alisema wakati mama huyo
akihudhuria kliniki walipojaribu kupima miezi ya mwisho mama huyo, mkao
wa mtoto ulikuwa haupatikani pamoja na mapigo ya moyo lakini mtoto
alikuwa anacheza tumboni jambo ambalo lilikuwa likiwashangaza waganga na
wauguzi kituoni hapo.
Dk Kihura alisema mara baada ya mama huyo kufanyiwa upasuaji waliweza
kutoa mtoto wa jinsi ya kike ambaye alikuwa na sura isiyoeleweka na
kichwa kilikuwa na sura ya binadamu na nusu ikiwa ni sura inayofanana na
chura huku viungo vingine vyote vya mwili vikiwa kamili.
Alisema zipo sababu kadha zinazoweza kusababisha tatizo kama hili
ambapo alisema kuwa ni baadhi ya akinamama kukosa baadhi ya madini
mwilini na uumbaji kutokamilika kutokana na sababu za kibaiolojia.
Alieleza kuwa hali ya mama huyo inaendelea vizuri na kwamba mtoto huyo alikuwa ni mtoto wake wa tano. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza
kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Na Habari Leo
No comments:
Post a Comment