Uingereza inaandaa sheria kupambana na ugaidi, kuzuia ongezeko la Waingereza wanaokwenda kupigana nchini Syria na Iraq.
Waziri
Mkuu wa Uingereza David Cameron ameelezea kwa mara ya kwanza sheria
hiyo inayopendekezwa yenye lengo la kuzuia ongezeko la Waingereza wenye
itikadi kali wanaokwenda katika nchi hizo.Waziri mkuu wa Uingereza ametangaza pendekezo la muswada huo katika hotuba yake aliyoitoa kwenye bunge la Australia mjini Canberra.
Katika sheria hiyo, amesema polisi wamepewa uwezo mpya kuweza kukamata hati za kusafiria za wanaodhaniwa kuwa wapiganaji wapya walioandikishwa na kundi la Islamic State, ambao wanajaribu kuondoka nchini humo.
''... Uwezo mpya waliopewa polisi katika bandari kukamata hati za kusafiria, kuwazuia washukiwa kusafiri na kuzuia raia wa Uingereza wanaorejea nchini humo isipokuwa tu wamefuata masharti yetu. Sheria mpya kuyazuia mashirika ya ndege ambayo hayata tii hatua zetu za kuwachunguza wasafiri, kuingia nchini Uingereza. Alisema Cameron.
Sheria hiyo inayopendekezwa pia itayatoza faini mashirika ya ndege ambayo hayatachukua hatua zaidi kuchunguza orodha ya abiria inayowabeba.
Serikali ya Uingereza inatarajia mswada huo utapitishwa kuwa sheria ifikapo mwishoni mwa Januari mwakani. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment