Rais Jakaya Kikwete akiagana na daktari bingwa, Edward Schaeffer baada
ya kuruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Johns Hopkins, Baltimore nchini
Marekani, alikofanyiwa upasuaji mwishoni mwa wiki iliyopita.
Rais Jakaya Kikwete ametoka
wodini katika Hospitali ya Johns Hopkins na kuhamishiwa kwenye hoteli
maalumu ambako ataendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.
Rais Kikwete alifanyiwa upasuaji wa tezi dume wiki iliyopita na afya yake imekuwa ikiimarika siku hadi siku.
Makundi mbalimbali ya wananchi yamekuwa yakimtakia
uponaji wa haraka kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu. Miongoni mwa
waliomtakia afya njema ni familia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius
Nyerere ambayo imeeleza kupokea kwa masikitiko taarifa za kuugua kwake
na kumwombea apone haraka ili aendelee na majukumu yake kwa Taifa.
Chama cha RPP cha Rwanda kimemtumia salamu za pole
Rais Kikwete na kuungana na mamilioni ya Watanzania kumwombea ili
arejee katika afya yake na majukumu ya kila siku. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
“RPP tutashirikiana na familia, marafiki na
mamilioni ya Watanzania kumwombea Rais Kikwete aweze kupona haraka. Rais
Kikwete ni jirani yetu na mtetezi mkubwa wa kanda hii katika kupata
ukombozi wa kijamii, kisiasa na kiuchumi,” ilisema taarifa ya RPP kwa
umma iliyotolewa na Rais wa chama hicho, John V Karuranga.
Aondoka wodini
Wakati Rais Kikwete akiondoka wodini, alikuwa
anatembea akiwa amesindikizwa na daktari bingwa, Edward Schaeffer kutoka
Hospitali ya Johns Hopkins na mkewe Salma.
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu
iliyotolewa juzi ilisema: “Afya yake imekuwa inaimarika kiasi cha
kuanza mazoezi ya kutembea na akiwa katika hoteli hiyo, ataendelea kuwa
chini ya uangalizi wa madaktari.”
Iliongeza: “Rais Kikwete ataendelea kupatiwa
matibabu, kutembelewa mara kwa mara na madaktari na kuwa chini ya
uangalizi wa wauguzi muda wote. Wiki moja baadaye, Rais Kikwete
atafanyiwa tathmini ya kuwawezesha madaktari kuamua hatua inayofuata ya
matibabu yake.”
Taarifa hiyo ilisema: “Kutokana na kuondolewa kwa
bandeji kwenye mshono ambao nao umeanza kukauka vizuri, Rais Kikwete
atakuwa katika hoteli maalumu (haikutajwa), iliyo na uhusiano na
Hospitali ya Johns Hopkins.” Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment