Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
amemtaka Rais Jakaya Kikwete kulivunja Baraza la Mawaziri na kuunda
jipya kutokana na tuhuma za ufisadi.
Katika taarifa yake aliyoitoa jana kwa vyombo vya
habari baada ya mikutano yake katika mikoa ya Magharibi alisema ni
lazima hatua hiyo kuchukuliwa ili kukabiliana na mafisadi ambao
hakuwataja, vinginevyo alisema Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
anayoiongoza, itaanza maandalizi ya kuwasilisha bungeni, hoja ya
kutokuwa na imani naye.
Alisema Serikali imekuwa ikishindwa kuchukua hatua
za ufisadi ambazo zinawakabili watendaji wake: “Kambi ya Upinzani
Bungeni inamtaka Rais Kikwete kumfukuza kazi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
na mawaziri wake na kuunda Serikali mpya.” Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Hivi karibuni, Mbowe alitoa tuhuma nzito kuhusu
ufisadi katika ujenzi na bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es
Salaam akisema kuna ufisadi umefanywa na vigogo wa Serikali wakiwamo
baadhi ya mawaziri.
Alisema mradi huo ulitakiwa kugharimu Sh1.2
trilioni lakini vigogo hao wakaongeza kiasi kama hicho na sasa
unagharimu Sh2.4 trilioni. Alitaka kuteuliwa kwa taasisi ya kimataifa ya
ukaguzi ili kufahamu thamani halisi ya ujenzi wa bomba hilo.
Alisema kutokana na ufisadi huo na mwingine katika
Akaunti ya Tegeta Escrow, ni dhahiri kuwa Baraza la Mawaziri
limeshindwa kazi ya kumsaidia Rais.
Mbowe amnanga Zitto
Katika mkutano wa juzi mjini Kigoma, Mbowe
alimzungumzia aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe
akisema alimsaidia kuhakikisha anashinda ubunge wa Kigoma Kaskazini
mwaka 2005 lakini akakosa shukrani.
Akihutubia mamia ya wakazi wa Kata ya Kalinzi
iliyopo katika Jimbo la Kigoma Kaskazini, Mbowe alisema hamchukii Zitto
kama baadhi ya watu wanavyofikiri, bali mbunge huyo alikiuka maadili ya
chama hicho akavuliwa uongozi. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
“Nilimshauri Zitto Kabwe akagombee katika Jimbo la
Kigoma Kaskazini, lakini akaniambia kwamba hawezi kufanya hivyo kwa
sababu hana fedha, nikampa fedha za kutosha, nikampa gari Toyota Hilux
la kuzungukia katika jimbo na akawa mbunge.
Alisema gari hilo hajawahi kulirudisha hadi leo na
yeye hakumuuliza kwa sababu alimchukulia kama ndugu yake... “Zitto ni
kama mdogo wangu, amelala na kula nyumbani kwangu, nyumba yangu ilikuwa
kama yake, nashangaa anakosa shukrani.”
Alisema kabla ya kugombea alimlipia nauli kutoka
Ujerumani kurudi nchini kwa ajili ya kutafuta nafasi hiyo ya ubunge,
hivyo anashangaa mtu wa aina hiyo amchukie kwa lipi.
Mbowe alisema Mkoa wa Kigoma umebahatika kuwa viongozi wa
upinzani wenye uwezo lakini wamekuwa wakiwasaliti wananchi wa mkoa huo.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum
Mwalimu alisema uchaguzi wa serikali ya vijiji, mitaa na vitongoji kiwe
kipimo cha kuing’oa CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Aliwataka vijana kufanya uamuzi sahihi kwenye uchaguzi huo kwa kuvichagua vyama vinavyounda Ukawa kwa kuwa CCM imewatelekeza.
Zitto ajibu
Akizungumzia madai ya Mbowe, Zitto alisema ni
utoto kwenda kumtangaza kwamba alimsaidia... “Yeye Mbowe anajua
nilivyomsaidia pia lakini kwa kuwa nimelelewa kwa maadili mema na wazazi
wangu siwezi kumtangaza. Ila muulizeni alikuwa na hali gani baada ya
uchaguzi wa mwaka 2005 na nilimsaidia nini?
“Nimeshangazwa na tabia hiyo ya kusimanga tena
kunisimanga kwetu, nyumbani kwetu. Hata hivyo, nimepuuza maana kwa
vyovyote vile aliongea bila kufikiri.
“Anasema nilitaka kusaliti chama, aseme kwa ushahidi maana kutamka tu hakuna maana kitu hata kidogo.”
Alisema kiongozi mkubwa kama Mbowe anapaswa
kujadili masuala ya Taifa na namna ya kutatua changamoto si, kusema watu
na kuwasimanga.
“Nimeibadilisha Kigoma na kusimamia ujenzi wa
miundombinu ya barabara, madaraja na viwanja vya ndege. Yeye kafanya
nini Hai? Nimewezesha wakulima wangu kuwa na hifadhi ya jamii, bima ya
afya na kukuza uzalishaji, yeye kafanya nini Hai?
Nimeibua hoja bungeni za maana ikiwamo kubadili
sheria kwa manufaa ya nchi. Yeye kafanya nini bungeni tangu aingie,
ametoa hoja gani binafsi, ametunga sheria gani binafsi? Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment