Kiongozi wa Kanisa
Katoliki duniani, Papa Francis amekubali kumuondolea sakramenti ya
upadri, Raymond Mosha wa Jimbo Katoliki la Moshi ikiwa ni miaka 20 tangu
padri huyo aombe kuachana na daraja hilo.
Barua ya uamuzi wa Papa Francis ilisomwa juzi
katika parokia na vigango vyote vya Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi
katika ibada zilizofanyika katika makanisa ya jimbo hilo.
Miongoni mwa parokia ambazo barua hiyo ilisomwa ni
Karanga ambako Paroko wake, John Matumaini alitoa tangazo hilo katika
ibada zote. Uamuzi huo ambao ni nadra kutolewa na Papa, unamaanisha kuwa
sasa padri huyo yuko huru kuoa na kuwa na familia.
Hata hivyo, wakati uamuzi huo ukitangazwa rasmi
juzi, tayari Padri Mosha ambaye ni profesa wa falsafa na maadili katika
Chuo Kikuu cha Nelson Mandela Arusha, ana mke na watoto watatu ambao kwa
sasa wako vyuo vikuu.
Padri Mosha alisema aliandika barua kuomba kuondolewa daraja hilo mwaka 1994 kabla ya uamuzi kutolewa juzi.
Katika orodha ya mapadre 185 wa Kanisa Katoliki
Jimbo la Moshi iliyopo katika tovuti ya jimbo hilo, jina la Padri Mosha
linaonekana likiwa ni namba 23.
Akizungumzia hatua hiyo, Padri Mosha alisema:
“Ninafurahi kufunguliwa kifugo hiki na hii itanifanya niishi kama
Mkristo. Kwa vile hawajaniondolea sifa ya kutoa huduma kama vile ibada
za mazishi, sakramenti ya mwisho na ubatizo, nitaendelea kutoa kwa
wahitaji kwa sababu ninaupenda ukristo.
“Nashukuru sasa nimekuwa muumini wa kawaida
nitaweza kufunga ndoa kanisani kwa kuwa nilikuwa nimefunga ndoa ya
kisheria tu kwa DC.”
Kuhusu kwa nini aliamua kuacha upadri, Profesa
Mosha alisema ni baada ya kufanya kazi hiyo kwa miaka 20 na akaona ipo
haja ya kuwa na familia lakini kanisa lilikuwa haliruhusu.
“Sasa kwa kuwa kanisa haliruhusu mapadri kuoa
ndiyo maana nikaamua kuandika barua ambayo hata hivyo, imechukua muda
mrefu kujibiwa na tayari nina watoto watatu wako chuo kikuu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment