WAKATI
uongozi wa Yanga ukidai hauna muda kuendelea kulijadili suala la
mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi, mshambuliaji huyo
naye amesema hana mpango wa kurudi kucheza soka Tanzania.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kupitia ukurasa wake wa
Facebook, Okwi alisema hana mpango wa kurudi nchini kwa sasa, kwani
anachoangalia ni kucheza soka barani Ulaya na sio Tanzania.
Awali, Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu, alikaririwa akisema,
wanachoangalia wao kwa sasa ni wachezaji gani wamefika na maendeleo yao
katika mazoezi, sio kumfuatilia yule ambaye hajafika.
Okwi inadaiwa kwa anaidai Yanga zaidi ya sh. milioni 60 zilizotokana
na fedha zake za kusajiliwa akitokea Etoile du Sahel ya Tunisia, huku
akisaini mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya sh. milioni 160.
Hata hivyo klabu hiyo inatakiwa kuvunja mkataba na mchezaji mmoja wa
kimataifa kutokana na kuzidi kwa idadi ya wachezaji watano wa kigeni
kama zinavyotaka sheria za usajili wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Wachezaji wengine wa kimataifa waliopo katika klabu hiyo ni Andrey
Coutinho, Geilson Santos ‘Jaja’ raia wa Brazil, Mbuyu Twite wa Burundi,
Hamis Kiiza wa Uganda na Haruna Niyonzima wa Rwanda. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment