Kikosi cha kiislam cha kijeshi
chenye msimamo mkali kimeachilia video inayoonesha mauaji ya mwandishi
habari mwenye asili ya Marekani. James Foley alipotea tangu alipokamatwa
mateka na kushikiliwa nchini Syria miaka miwili iliyopita na sasa
ameuawa.
Ikulu ya Marekani imesema inaifanyia uchunguzi
wa kina video hiyo na ikithibitika kwamba mwandishi huyo wa habari ni wa
taifa hilo ,serikali ya Marekani itataka ufafanuzi wa kina ilikuaje na
kwanini James Foley auawe.Katika mtandao wa kijamii wa Facebook familia ya mwandishi huyo iliandika kuwa’tunajua kwamba wengi wenu mnasubiri uthibitisho ama majibu ya maswali yenu,tafadhalini muwe watulivu mpaka nasi sote tupate taarifa tunazo tamia,na tunaomba muendelee kumbumbuka Foleys na kumwombea kila siku.’’
Katika video hiyo iliyobeba ujumbe unaosomeka kua ujumbe kwa Marekani,mwandishi huyo pia alionekana akiwa chini ya ulinzi wa mtu aliyekua amevalia kinyago usoni,askari huyo alikua aku akizungumza ndani ya lafidhi yenye athari za Uingereza,akisema kua kifo cha mwandishi huyo ni matokeo ya mashambulizi ya magurunedi yalowalenga wa Iraq. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment