MWELEKEO
mpya wa mchakato wa Katiba mpya, adhabu kwa wagombea walioanza mbio za
kusaka urais unatarajia unatarajia kujulikana leo baada ya kumalizika
kwa kikao cha Kamati Kuu (CC), ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
CC ilikutana jana chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete, ambaye
alisema hana ajenda mfukoni kama ilivyodaiwa na baadhi ya watu.
“Nimekuja, Tuzungumze mambo yetu, tufanye uamuzi…..hivi mara ya
mwisho kukutana ilikuwa lini vile….aah mwezi uliopita” alisema mambo
yetu.
Kikao hicho cha CC ambacho kilikuwa kianza saa nane mchana kama
ilivyotangazwa kilianza saa tisa na nusu huku wajumbe wote wakiwa tayari
ndani ya ukumbu isipokuwa viongozi wakuu.
Viongozi hao wakuu ni Rais Kikwete (Mwenyekiti), Katibu Mkuu
Abdulrahman Knana, Makamu Mwenyekiti (bara), Philip Mangula na Makamu
Mwenyekiti (Zanzibar) Dk. Alli Mohamed Shein.
Kabla ya Rais Kikwete, kuingia ukumbini Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana, alitoka faragha alikokuwa akizungumza na kwenda
kuchukua nyaraka kwa Jenister Mhagama ambaye ni Katibu wa wabunge wa CCM
na kurejea faragha ambapo alikaa kidogo kisha kurejea ukumbini kumuita
Dk. Asharose Migiro.
Mara baada ya pilika pilika hizo, Rais Kikwete na viongozi wenzake
waliokuwa faragha waliingia ukumbini ambapo Kinana alimkaribisha Rais
Kikwete afungue mkutano huo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Kabla ya kuanza kwa kikao hicho Tanzania Daima, lilidokezwa kuwa
kikao hicho kinaweza kufanya uamuzi wa kumteua Dk. Emmanuel Nchi kuwa
Naibu Katibu Mkuu kuchukua wadhifa wa Mwigulu Nchemba, aliyeteuliwa kuwa
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi.
Pia nafasi nyingine ambayo inaweza kujazwa ni ya Katibu wa Siasa na
Mambo ya Nje, Dk. Migiro, aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Tanzania Daima, pia limedokezwa katika kikao hicho wajumbe watapata
nafasi ya kujadili mwenendo wa makada wake iliyowaadhibu kwa kuanza
kampeni za kuwania urais kabla ya wakati.
Makada hao waliofungiwa mwaka mmoja mwanzoni mwa mwaka huu ni
Mawaziri wastaafu, Fredrick Sumaye, Edward Lowassa, Berbard Membe,
Stephen Wasira, William Ngeleja na January Makamba.
Tanzania Daima, lilidokezwa CC inaweza kuwaongezea adhabu baadhi ya
makada wanaodaiwa kuendelea kukiuka masharti ya adhabu waliyopewa.
Kikao hicho cha CC kimefanyika huku kukiwa na vuguvugu ndani na nje
ya chama hicho la kutaka Bunge Maalum la Katiba, lisitishe vikao vyake
kwasababu ya kukosekana kwa maridhiano baina ya CCM na vyama vinne
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Tanzania Daima, lilidokezwa baadhi ya makada wa CCM wanataka Bunge
hilo liahirishwe hadi wafikie maridhiano na Wajumbe wa Umoja wa Katiba
ya Wananchi (UKAWA), waliosusia vikao vyake.
Wanaotaka Bunge hilo liahirishwe wanajenga hoja kuwa kutokuwapo kwa
UKAWA kutaikosesha uhalali wa kisiasa Katiba mpya iwapo wananchi
wataridhia kilichopendekezwa na Bunge.
Wanaopinga kuahirishwa kwa Bunge akiwemo Mwenyekiti wa Bunge hilo
Samuel Sitta, wamejikita kwenye sheria na kanuni zinazowaruhusu
kuendelea na vikao hivyo.
Kundi hili linaona kusitishwa kwa Bunge kutakuwa pigo kwao na chama hasa kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani.
Wanajenga hoja kuwa iwapo litasitishwa hivi sasa wapinzani wanaweza
kutumia turufu hiyo kuilaumu CCM kutumia mabilioni ya fedha za umma
wakijua awamu ya pili Bunge hilo haitofanikiwa bila UKAWA.
Tanzania Daima, imedokezwa kuwa tathimini ya CC ndiyo itakayoamua majaaliwa ya mchakato huo uliowagawa Watanzania.
Kuna Watanzania wasiotaka mchakato huo usitishwe hadi baada ya
uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani ingawa wengine wakitaka liendelee.
Tayari kuna wasiwasi wa kuwa Bunge Maalum linaweza lisitoe katiba
inayotakiwa hasa baada ya dalili za kukwama kwake zikianza kuonekana
katika zoezi la upigaji kura.
Kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya Katiba na Katiba ili mabadiliko
yoyote yanayohusu masuala ya muungano yanahitaji kupata uungwaji mkono
wa theluthi mbili ya wajumbe wote kutoka Zanzibar na idadi hiyo hiyo kwa
Tanzania bara.
Wasiwasi wa kukwama huko kumeshaonyeshwa na wajumbe wa Bunge Maalum
akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa CCM (bara), Mwigulu Nchemba aliyetaka
ifanyike tathmini ya mahudhurio ya wajumbe.
Mwigulu alitaka kama itathibitika Bunge hilo halitokuwa na uwezo wa
kupitisha maamuzi mwishoni ni vema likasitishwa ili fedha za Watanzania
ziokolewe.
Hata hivyo baadhi ya makada wa CCM walimlaumu Mwigulu kutoa kauli huyo bungeni badala ya kwenye vikao vya chama.
Walijenga hoja kuwa kauli ya kiongozi huyo wa chama na Naibu Waziri wa Fedha imezidisha utete wa mchakato wa Katiba mpya.
Pia walimlaumu kwa kujitafutia huruma za Watanzania kufanikisha
dhamira yake ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika
mwakani.
Hata hivyo Tanzania Daima, lilidokezwa kuwa baadhi ya wajumbe wa
Bunge Maalum hawataki kusitishwa kwa Bunge hilo ili waendelee kupata
posho ya sh 300,000 inayotolewa kwa siku kwa atakayehudhuria vikao. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Kutokana na msuguano huo, tathimini ya CC inatarajia kutoa mwanga mpya wa mchakato wa Katiba mpya.
Itakumbukwa mwanzoni mwa wiki hii, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji
Fredrick Werema alisema kama Katiba mpya haitopatikana Bunge litafanya
marekebisho ya 15 ya Katiba.
Alisema marekebisho hayo yatalenga kuruhusu tume huru ya uchaguzi, mgombea binafsi na matokeo ya urais kuhojiwa mahakamani.
Mivutano
Wakati CC, ikifanya tathimini ya vikao vya Bunge Maalum, Kamati
mbalimbali za Bunge hilo ziliendelea na vikao vyake huku mivutano ikiwa
kwenye muundo wa mahakama, Bunge, viti maalum na ukomo wa Bunge.
Kamati namba tano inayoongozwa na Hamad Rashid Mohamed, ilipinga
pendekezo la rasimu ya katiba lililokuwa likitaka ukomo wa Bunge uwe wa
miaka 15.
Pia kamati hiyo ilipendekeza kufutwa kwa viti maalum na kuanzisha
dirisha jingine ambalo hakutaka kulitaja lakini alisema litasaidia
kuondoa upendeleo na kujua katika viti maalum.
Hamad alisema k,uwa pia wajumbe wengi wa kamati yake wamependekeza
utaratibu wa sasa wa wabunge wa Zanzibar waendelee kushiriki kwenye
vikao vya Bunge la Jamuhuri na kujadili hata masuala yasiyohusu
muungano.
Mahudhurio
Mahudhurio katika kamati nyingi yameendelea kuwa ya kusuasua hali
iliyozifanya baadhi ya kamati kuchelewa kuanza vikao vyake na nyingine
kuahirisha zoezi la upigaji kura wa ibara husika.
Kamati namba tatu jana ililazimika kuahirisha kikao chake kwa muda na
kuwaruhusu wajumbe wake wajisomee nyaraka ili kusubiri wajumbe wengine
ili watimize akidi.
Jhata hivyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dk. Francis Michael, alisema
aliwaruhusu wajumbe wake wajisomee si kwakuwa akidi haitimii bali kutoa
muda wa kusoma kwa kina nyaraka zao.
Naye Katibu wa Bunge Maalum, Yahya Khamis Hamad, alisema mpaka jana
wabunge 441 kati ya 630 ndiyo waliojiandikisha kuhudhuria vikao hivyo.
“Kimsingi majadiliano kwenye kamati za Bunge yanaendelea vizuri…, tuna imani Katiba mpya itapatikana” alisema. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment