Tuesday, May 03, 2016

MAGAZETI YA LEO JUMANNE MEI 03, 2016 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

20160503_082607 20160503_082619 20160503_082640
Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

WAZIRI MAHIGA AMTETEA MKEWE

Dk. Augustine Mahiga 

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga, amezungumzia sakata la mke wake kudaiwa kumtukana askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani.

Akizungumza na mwwandishi wa habari hii jana mjini hapa, Dk. Mahiga alisema kwamba mke wake alipishana kauli na askari huyo aliyefahamika kwa jina la Deogratius Mbango, na hakutoa lugha ya matusi kama inavyodaiwa.

Alisema baada ya kupokea taarifa hiyo, alifuatilia ili kujua ukweli, ikiwamo kusikiliza sauti ya majibizano baina ya askari huyo na mkewe, ambapo alibaini kuwa walipishana kauli. Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

UKAWA WANUSA JIPU OFISI YA MAKAMU WA RAIS



CAG


KAMBI Rasmi ya Upinzani Bungeni, imeibua ufisadi wa zaidi ya Sh bilioni tisa katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), unaohusisha fedha zilizotolewa na wafadhili kwa ajili ya miradi ya mazingira katika maeneo ya Dar es Salaam, Bagamoyo, Pangani, Rufiji na Zanzibar.

Kambi hiyo imeeleza kushangazwa na hatua ya Serikali kuomba tena kiasi hicho cha fedha katika bajeti ya mwaka 2016/17, kwa ajili ya kazi hiyo hiyo ambayo fedha zake zilishatolewa na nchi wahisani ambazo ni Marekani na Ujerumani.

Kwa mujibu wa kambi hiyo, miradi hiyo miwili ilikumbwa na ufisadi mkubwa ambao ulikuwa ukiendeshwa baina ya mtumishi mmoja aliyeko katika Ofisi ya Makamu wa Rais Idara ya Mabadiliko ya Tabianchi akishirikiana na kigogo mmoja aliyekuwa Ikulu wakati wa utawala wa awamu ya nne. Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

MTOTO WA MWAKA MMOJA AOKOLEWA AKIWA HAI KWENYE KIFUSI KENYA

Mtoto wa umri wa mwaka mmoja unusu amepatikana akiwa hai kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka Ijumaa jijini Nairobi. Jengo hilo la ghorofa sita liliporomoka katika mtaa wa Huruma baada ya mvua kubwa kunyesha.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, msichana huyo alitolewa kwenye vifusi mwendo wa saa kumi usiku na kukimbizwa hospitalini. Kamanda wa kitengo cha taifa cha kudhibiti majanga Pius Maasai anasema hali ya mtoto huyo ni thabiti, kwa mujibu wa gazeti hilo. Watu 22 wamethibitishwa kufariki na wengine karibu 90 hawajulikani walipo. 

Juhudi za uokoaji bado zinaendelea siku ya nne baada ya mkasa huo kutokea. Kufikia sasa, watu 136 wameokolewa. Polisi wanasema wamiliki wa jumba hilo, ambalo maafisa wa baraza la jiji wanasema halikufaa kuishi watu, wamekamatwa na wanazuiliwa na polisi. Taarifa zinasema watafikishwa mahakamani baadaye Jumanne. Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

BRAZIL YAZUIA MATUMIZI YA WHATSAPP KWA MASAA 72


Wananchi wa Brazil watakosa huduma ya WhatsApp katika simu na vifaa vingine kwa siku tatu kufuatia kufungwa kwa matumizi ya app hiyo ikiwa ni kama adhabu kwa mmiliki wa WhatsApp.

Hatua ya kufungiwa kwa WhatsApp imetolewa na Jaji mmoja nchini humo, Marcel Montalvao kwa madai kuwa mmiliki wa WhatsApp ambaye pia ndiyo mmiliki wa Facebook ameshindwa kutoa taarifa za mtumiaji wa mtandao katika kesi iliyo mahakamani.

Kufungwa kwa huduma hiyo kulianza jana 17:00 ambapo hakutakuwa na huduma hiyo kwa masaa 72 na baada ya hapo huduma itarejea kama awali. Baada ya kufungiwa, WhatsApp nao wamejibu kuwa wanashangazwa na jambo hilo kuwanyima wateja wao huduma yao kwa taarifa ambayo wameshaitolea majibu.

“Haya maamuzi ya kuwaadhibu zaidi ya Wabrazil milioni 100 ambao wanatumia huduma zetu kwa ajili ya kutulazimisha sisi kutoa taarifa, tunarudia tena hatuna hiyo taarifa,” ilisema taarifa hiyo. Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

MAELFU WAMUAGA PAPA WEMBA, KUZIKWA KESHO JUMATANO

Mwili wa mwimbaji nguli wa muziki wa dansi nchini DR Congo, Papa Wemba, ambao upo ndani ya Nchi hiyo jana na leo maelfu wamejitokeza kuuaga mwili na kutoa salamu zao na unatarajia kuzikwa kesho siku ya Jumatano 04 Mei 2016. 

Maelfu ya waombolezaji hao walijitokeza kuadhimisha misa ya wafu kwa heshima ya mwanamuziki nyota huyo wa muziki wa Soukus na Rhumba. Tayari Serikali imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia leo hadi jumatano atakapozikwa kijijini kwao Molokai na utalala kijijini kwake leo na taratibu za mazishi hiyo kesho.
PAPA WEMBA 
Mwili wa Papa Wemba ukitembezwa mitaa mbalimbali ya Jiji la Kinshasa DR Congo.
Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.
13071951_1144833132213632_7462765191070434206_o
Kwa ratiba hiyo inaonyesha  baada ya mwili huo kulala kwa siku moja katika kijiji cha Papa Wemba na kuendelea na sara na mambo ya mila na kufuatia maziko Papa Wemba alifariki hivi karibuni jijini Abidjan nchini Ivory Coast ambapo awali alipoteza fahamu akiwa jukwaani alipokuwa akitumbuiza baada ya kuanguka na kukimbizwa hospitali.

KOCHA WA AZAM ALAUM WACHEZAJI WAKE

KOCHA msaidizi wa Azam FC, Denis Kitambi, amewatupia lawama washambuliaji wake kwa kushindwa kufuata maelekezo ya walimu, kiasi cha kuyumbisha mwenendo wa timu hiyo katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kitambi aliyasema hayo baada ya kumalizika kwa mchezo wao na Simba na timu hizo kutoka sare ya 0-0, katika mechi ya ligi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kitambi alisema, sare hiyo imefifisha mbio zao katika kuwania taji la Ligi Kuu linaloshikiliwa na Yanga.

“Washambuliaji wetu wana kiwango kizuri, lakini hakuna faida ya kuonyesha uwezo bora ikiwa unashindwa kuipatia timu yao mabao. Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

LEICESTER CITY MABINGWA WAPYA EPL

Klabu ya soka ya Leicester City wameshinda taji la ligi kuu England katika historia inayovutia kwenye ligi hiyo. Suluhu ya 2-2 waliyoipata Tottenham dhidi ya Chelsea siku ya jumatatu usiku ilisababisha mafanikio hayo makubwa kuwahi kutokea kwa upande wa Claudio Ranieri.

Leicester walianza kampeni zao za ubingwa huku wakipewa nafasi moja tu kati ya 5000 kushinda taji la ligi na pia wakitoka katika janga la kutaka kushuka daraja. Lakini wamepoteza michezo mitatu tu katika kile kinachotafsiriwa kama hadithi za kale na ushindi wa kipekee katika timu hiyo. 

Wapinzani wao wa karibu Spurs, Arsenal,Manchester City, Manchester United na washindi wa ligi msimu uliopita Chelsea wameshindwa kuwazuia mbweha katika msimu mzima wa ligi.

Sunday, May 01, 2016

MWILI WA MAMA LUCY KIBAKI WAWASILI NCHINI KENYA

 Mama Lucy Kibakienzi za uhai wake.
Mwili wa mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai kibaki , mama Lucy Kibaki umewasili leo alfajiri mjini Nairobi ukitokea London Uingereza na kutumbukiza taifa zima katika kipindi cha maombolezi.

Mabaki ya bi Kibaki yalilakiwa katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta na rais Uhuru Kenyatta Naibu wake William Ruto na viongozi na wakenya wa haiba mbalimbali mwendo wa saa kumi na moja. Ndege iliyoileta familia ya rais Kibaki ilitua saa kumi na moja na dakika tatu na kupewa hadhi ya kitaifa.

AL SHABAB WAUA WANAJESHI 30 WA SOMALIA

Wanamgambo wa Al Shabab.
Wapiganaji wa Kiislamu wa Somalia, Al Shabab wanasema wamewauwa wanajeshi wa serikali zaidi ya 30. Al Shabab, wanadai kutekeleza mauaji hayo walipoteka tena kijiji cha Runorgood, Kaskazini-Mashariki mwa mji mkuu wa Somali Mogadishu.

Wenyeji wa kijiji hicho wamethibitisha, kwamba kijiji chao kinadhibitiwa tena na wanamgambo wa Al Shabab.
Wanamgambo wa Al Shabab.
Wapiganaji hao walikuwa wametimuliwa kutoka kijiji hicho hapo jana. Kwengineko nchini Somalia, watu kama watatu waliuwawa, kwenye shambulio la bomu, katika soko la mifugo huko Qoryoolay, inavoelekea shambulizi hilo lililengwa maafisa wa kukusanya kodi wa serikali.

SIMBA, AZAM ZATOKA SARE YA BILA KUFUNGANA

SIMBA SC imelazimisha sare ya bila kufungana na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Matokeo hayo yatapokewa kwa furaha na mahasimu, Yanga ambao sasa wanaongoza Ligi Kuu kwa wastani wa pointi sita kuelekea mechi nne za mwisho. Kwa sare hiyo ya 0-0, Azam FC inafikisha pointi 59, wakati Simba sasa inakuwa na pointi 58, nyuma ya mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 65 baada ya timu zote kucheza mechi 26.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Mathew Akrama wa Mwanza, aliyesaidiwa na washika vibendera Abdallah Mrisho wa Pwani na Omar Kambangwa wa Dar es Salaam hakukuwa na mashambulizi ya kusisimua na timu zote zilionekana kucheza kwa tahadari kupita kiasi, hivyo kuufanya mchezo upooze. 

Saturday, April 30, 2016

WAZIRI MKUU "TUTAUFANYIA KAZI USHAURI WA WAZIRI MKUU"

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imeupokea na itaufanyia kazi ushauri wa Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe aliyetaka Benki ya Standard ICBC ya Uingereza na kampuni dada ya Stanbic Tanzania kuchunguzwa juu ya mkopo wa hatifungani wa Sh1.2 trilioni ambao umegubikwa na ufisadi.

Zitto alitoa kauli hiyo juzi wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Rais-Tamisemi na Utawala Bora mwaka 2016/17 na kutaka Bunge liunde kamati teule kuchunguza suala hilo na ukweli ukibainika, Serikali itakwepa kulipa deni la Sh2 trilioni ambazo Tanzania inatakiwa kulipa ikiwa ni deni na riba.

Majaliwa alitoa kauli hiyo jana mjini Dodoma baada ya kuulizwa swali na waandishi wa habari juu na hatua ambazo Serikali imezichukua kutokana na sakata hilo linalodaiwa kuwa na harufu ya ufisadi, kwamba baada ya uchunguzi kukamilika taarifa itatolewa.

Tuesday, April 19, 2016

MAGUFULI ATINGA CRDB KAMA RAIA WA KAWAIDA...!!!

Rais John Pombe Magufuli akiondoka katika benki ya CRDB, Tawi la Holland baada ya kumaliza shughuli iliyompeleka.

Rais John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi mkono wakati akiondoka katika benki ya CRDB, Tawi la Holland. 

Wakati akikaribia kuingia ndani ilibidi baadhi ya wateja waliyokuwa wakijiandaa kuingia ndani ya benki hiyoi wazuiwe kuingia huku huduma ikiendelea tu kwa wale ambao waliyokwishaingia. Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.
Aidha, baada ya kuingia ndani baadhi ya wateja wa tawi hilo na wananchi wengine walibaki wakishangaa huku wengine wakijiuliza imekuwaje Rais kuingia benki kwa sitaili ile. Baadhi ya wananchi walisema hawajaona tukio kama lile kwa Marais wote waliyopita.

James Charles, ambaye ni dereva wa taxi, alisema baadhi ya wananchi waliyokuwa kwenye eneo hilo baada ya kuona ulinzi unaimarishwa walishituka na mara wakamuona Rais Magufuli akishuka kwenye gari, hali iliyowafanya wafikirie anakwenda kutembelea ofisi yake ya zamani.

“Lakini kufumba na kufumbua tukamuona anaelekea kwenye benki ya CRDB, tukajiuliza vipi rais leo kaamua kuwa kama mteja? Hata hivyo tujui kama hiyo ilikuwa inawezekana. Lazima kutakuwa na kitu. Haiwezekani aende akachukue fedha kwa utaratibu ule. Ngoja tusubiri tutasikia amefuata nini,” alisema Charles.

Joyce Godwin ambaye ni mwanafunzi wa chuo kimojawapo cha elimu ya juu alisema kuja kwake kumewashtua wafanyakazi wa tawi la benki hiyo kwani walidhani alikwenda pale kwa ajili ya kutumbua majipu.

“Mimi wakati Rais Magufuli anaingia nilikuwepo ndani kwenye foleni nikisubiri huduma. Kwa ujumla kila mmoja wetu alishituka lakini hatukujua kilichomleta,” alisema. Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

ANGALIA PICHA ZA MUONEKANO WA DARAJA LA JIPYA LA KIGAMBONI


Hatimaye ile ndoto ya muda mrefu ya Watanzania kuona daraja la Kigamboni likikamilika imewadia baada ya ujenzi ulioanza mwaka 2012 kukamilika na kesho Aprili, 19 linataraji kuzinduliwa na Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.


Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...