KOCHA msaidizi wa Azam FC, Denis Kitambi,
amewatupia lawama washambuliaji wake kwa kushindwa kufuata maelekezo ya walimu,
kiasi cha kuyumbisha mwenendo wa timu hiyo katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu
Tanzania Bara.
Kitambi aliyasema hayo baada ya kumalizika kwa
mchezo wao na Simba na timu hizo kutoka sare ya 0-0, katika mechi ya ligi
iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kitambi alisema, sare
hiyo imefifisha mbio zao katika kuwania taji la Ligi Kuu linaloshikiliwa na
Yanga.
“Washambuliaji wetu wana kiwango kizuri, lakini
hakuna faida ya kuonyesha uwezo bora ikiwa unashindwa kuipatia timu yao mabao. Tangaza
biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo
Tz. tu-follow instagram @jambotz.
“Tatizo hili limekuwa sugu sasa, tumejikuta
tukitengeneza nafasi nyingi za kupata mabao na kushindwa kuzitumia na hili
halijatokea kwenye mchezo huu tu, hata kwenye mechi za huko nyuma,” alisema
Kitambi.
Kitambi alisema wamekuwa wakijitahidi kulifanyia
marekebisho tatizo hilo wakitegemea kuona mabadiliko, lakini washambuliaji wao
wameendelea kuboronga.
Timu hiyo ambayo inashikilia nafasi ya pili
katika msimamo wa ligi ikiwa na jumla ya pointi 59, leo inatarajia kuendelea na
maandalizi ya mchezo wake ujao dhidi ya JKT Ruvu, ambao unatarajiwa kufanyika
kesho katika Uwanja wa Azam Complex, Chamanzi. Tangaza biashara yako hapa. Pia
like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram
@jambotz.
No comments:
Post a Comment