Siku kama ya leo mwaka
1996, ilikuwa ni vilio kila kona ya nchi, lakini Kanda ya Ziwa
iliathirika zaidi na kuzama kwa meli ya Mv Bukoba na kuteketeza mamia ya
wananchi.
Kuzama kwa Mv Bukoba inaelezwa ni kutokana na kuwa
ubovu. Tukio hilo ambalo haliwezi kufutika vichwani mwa wakazi wa Kanda
ya Ziwa, lakini kilio chao cha kupatiwa meli mpya licha ya Rais Jakaya
Kikwete kuahidi Serikali kununua mwaka 2010, haijanunuliwa hadi sasa.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa ujenzi wa meli hiyo
mpya iliyoahidiwa na Rais Kikwete kwa Ziwa Victoria unatarajia
kukamilika mwaka 2016.
Akizungumza ofisini kwake wiki hii, Ofisa Masoko
wa Huduma za Meli Mwanza Obedi Nkongoki alisema mjenzi wa meli hiyo
Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Denmark (Danida) kwa kushirikiana
na Serikali ya Tanzania.
“Ujenzi huu unahusisha meli nne ingawa Rais
aliahidi tatu; Ziwa Victoria moja, mbili Ziwa Tanganyika na nyingine
Ziwa Nyasa ambazo zinatarajiwa kukamilika 2018, huku ya Ziwa Victoria
ikitarajiwa kukamilika 2016,” alisema Nkongoki. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz