Mbunge
wa Kigoma Kaskazini kupitia Chadema Zitto Kabwe muda mfupi uliopita
kupitia kwenye ukurasa wake wa Facebook ametoa yake ya moyoni kwa hili
seke seke linaloendelea nchini juu Wafanyabiashara na Mamlaka ya Mapato
Tanzania[TRA]kuhusu mashine za kutolea risiti za EFD.
Zitto alianza kwa kuandika>>’EFD zilianza kutumiwa mwaka 2010
kwa jumla ya wafanyabiashara 16,000 waliosajiliwa kwenye Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT). Mwaka wa fedha 2009/2010, kabla ya EFD,
makusanyo ya kodi ya VAT yalikuwa tshs 791 bilioni’
‘Mwaka 2011/2012 makusanyo yaliongezeka kwa asilimia 40 mpaka tshs
1,086 bilioni. Mwaka 2012/2013 makusanyo yakaongezeka kwa asilimia 63
mpaka kufikia tshs 1,770 bilioni. Makusanyo haya ni kwa Wafanyabiashara
16,000′
‘Iwapo awamu ya pili ya EFD itatekelezwa bila vikwazo jumla ya
Wafanyabiashara 200,000 watafikiwa ikiwemo ni pamoja na vituo vya mafuta
(Petrol Stations), Mahoteli na Migahawa nk. Mamlaka ya Mapato
inatarajia kukusanya zaidi ya tshs 3,500 bilioni kutoka VAT peke yake
iwapo EFD zitatumika’
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz