Takriban wanajeshi 1,600 wa Ufaransa
na 6,000 wa Umoja wa Afrika wamo nchini humo kujaribu kulinda raia
wakati ghasia zenye maafa zikiendelea kati ya Wakristo na Waislam.
Waziri wa ulinzi wa Ufaransa anasema lazima tahadhari zichukuliwe ili Jamhuri ya Afrika ya Kati isigawanyike. Onyo hilo limetolewa huku makundi ya kutetea haki za binadamu yakionya kuwa mauaji ya kikabila yanaendelea katika taifa hilo lililokumbwa na mgogoro wa kisiasa.
Waziri huyo Jean Yves Le Drian alifanya mazungumzo mjini Bangui na maafisa wa ngazi ya juu ya jeshi la Ufaransa pamoja na kaimu rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Catherine Samba- Panza aliyeungana naye wakati wa ziara yake kusini magharibi mwa nchi.

Hii ni mara ya tatu kwa waziri Le
Drian katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, tangu Ufaransa ilipozindua
operesheni ya kijeshi mwishoni mwa mwaka jana. Onyo lake limetolewa huku
makundi mawili ya kutetea haki za binadamu Amnesty International na
Human Rights Watch yakionya juu ya mauaji ya kikabila katika baadhi ya
maeneo ya nchi yanayolenga waislam walio wachache.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Akizungumza na kituo cha televisheni
ya Ufansa France 24, kamishina wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya
wakimbizi Antonio Guterres alisema hali katika Jamhuri ya Afrika ya Kati
ni janga la kibinadamu. Alitoa mwito kwa jamii ya kimataifa kuongeza
idadi ya walinda amani haraka ili kurejesha uthabiti nchini humo.
Takriban wanajeshi 1,600 wa Ufaransa
na 6,000 wa Umoja wa Afrika wamo nchini humo kujaribu kulinda raia
wakati ghasia zenye maafa zikiendelea kati ya Wakristo na Waislam.
Jumuiya ya Ulaya inategemewa kupeleka wanajeshi 500 katika mji mkuu
Bangui mapema mwezi Machi.
Jumanne, Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa Ban Ki Moon alisema ameomba Ufaransa kupeleka wanajeshi zaidi
nchini humo kuzuia ghasia hizo kuendelea. Takriban watu 1,000 wameuawa
na maelfu kutoroshwa makazi yao.
No comments:
Post a Comment