Kampuni ya kutengeza magari ya Toyota
nchini Japan, imeagiza kurejeshwa kwa magari milioni 1.9 aina ya Prius katika kiwanda cha magari hayo nchini Japan.
Hii ni kutokana na hitilafu ya kimitambo ambayo inaweza kusababisha gari hilo kukwama.
Gari la Prius ni moja ya magari yenye muundo unaonyesha ubunifu wa hali ya juu wa kampuni ya Toyota.
Gari hilo linaweza kutumia petroli na betri huku likitoa kiwango kidogo sana cha moshi kuliko magari ya kaiwada.
Sasa kampuni hiyo imetambua hitilafu
ya programu ya gari hilo ambayo inaweza kusababisha vifaa vya
elektroniki vya gari hilo kukwama.
No comments:
Post a Comment