Mbunge
wa Kigoma Kaskazini kupitia Chadema Zitto Kabwe muda mfupi uliopita
kupitia kwenye ukurasa wake wa Facebook ametoa yake ya moyoni kwa hili
seke seke linaloendelea nchini juu Wafanyabiashara na Mamlaka ya Mapato
Tanzania[TRA]kuhusu mashine za kutolea risiti za EFD.
Zitto alianza kwa kuandika>>’EFD zilianza kutumiwa mwaka 2010
kwa jumla ya wafanyabiashara 16,000 waliosajiliwa kwenye Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT). Mwaka wa fedha 2009/2010, kabla ya EFD,
makusanyo ya kodi ya VAT yalikuwa tshs 791 bilioni’
‘Mwaka 2011/2012 makusanyo yaliongezeka kwa asilimia 40 mpaka tshs
1,086 bilioni. Mwaka 2012/2013 makusanyo yakaongezeka kwa asilimia 63
mpaka kufikia tshs 1,770 bilioni. Makusanyo haya ni kwa Wafanyabiashara
16,000′
‘Iwapo awamu ya pili ya EFD itatekelezwa bila vikwazo jumla ya
Wafanyabiashara 200,000 watafikiwa ikiwemo ni pamoja na vituo vya mafuta
(Petrol Stations), Mahoteli na Migahawa nk. Mamlaka ya Mapato
inatarajia kukusanya zaidi ya tshs 3,500 bilioni kutoka VAT peke yake
iwapo EFD zitatumika’
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
‘Wafanyabishara kote nchini wanalalamika. Mwanzoni hoja kubwa ilikuwa
ni bei za mashine hizi. Hoja inayoeleweka kabisa. Kamati ya PAC iliwahi
kushauri kuwa Wafanyabiashara wapewe bure kabisa mashine hizi (bila
kusubiri kurejeshewa kupitia kodi’
‘Kimsingi mashine hizi ni Bure isipokuwa Mfanyabiashara huikopesha
TRA na TRA kumrudishia kupitia kodi ya Mapato katika mwaka wa kwanza wa
matumizi).
Leo nimesoma kwenye vyombo vya habari wafanyabiashara wanataka mashine hizi zisitumike kabisa, mpango mzima ufutwe. Ni kweli Wafanyabiashara wa Tanzania hawataki kabisa mashine hizi?’
Leo nimesoma kwenye vyombo vya habari wafanyabiashara wanataka mashine hizi zisitumike kabisa, mpango mzima ufutwe. Ni kweli Wafanyabiashara wa Tanzania hawataki kabisa mashine hizi?’
‘Wafanyabiashara wanasema kodi ya VAT ya 18% ni kubwa mno na inakatwa
bila kuzingatia manunuzi yao ie gharama zao za uzalishaji. Siku zote
VAT inakatwa kutoka kwenye mauzo ghafi au kutoka faida?’
‘Hebu tujadili masuala haya na yale malalamiko ya msingi yafanyiwe kazi na yasiyo ya msingi yapuuzwe.
Tutaendelea kuwa Taifa tegemezi iwapo hatutaweza kujenga utamaduni wa kulipa kodi. Nchi hii haina mjomba………’.
Tutaendelea kuwa Taifa tegemezi iwapo hatutaweza kujenga utamaduni wa kulipa kodi. Nchi hii haina mjomba………’.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
No comments:
Post a Comment