WARAKA WA PAPII KOCHA
Mahakama hiyo ilikubali ombi hilo hivi karibuni na kueleza kuwa marejeo
hayo yanatarajiwa kusikilizwa Oktoba 30, mwaka huu ikiwa ni miezi
kadhaa baada ya Papii Kocha kutuma waraka wa kuomba msamaha kwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ndiye aliyekubali
kuufikisha kwa JK hivyo kuna madai kuwa huenda waraka huo ndiyo umezaa
matunda.
“Unajua ule waraka ulikuwa na maneno ya kuumiza sana. Inawezekana
kabisa kuwa ulimfikia JK akaagiza suala hilo liangaliwe upya. Haina
maana kuwa JK anaingilia sheria. Nadhani wanasheria wana vipengele vingi
ambavyo vinaruhusu marejeo ya rufaa hiyo. Kilichopo hapa ni namna ya
kuzitafsiri sheria kisha kuona kama rufaa hiyo inaweza kusikilizwa.