Rais
wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein wapili kushoto akiomba Dua pamoja na
viongozi wengine wa Kitaifa katika Swala ya Idi –El-Hjji ilioswaliwa
Kitaifa huko katika kitongoji cha Marumbi Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati
Unguja.kulia kwake ni Kadhi Mkuu wa Zanzibar Khamis Haji Khamis na
kushoto yake ni Katibu mtendaji wa Wakfu na Mali ya Amana Sheikh Abdalla
Twalib,Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanizbar Maalim Seif Sharif Hamadi
na wamwisho ni Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmod Mussa Wadi.
Rais
wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akitoa hotuba katika baraza la Idi
-El-Hajji lililofanyika huko Tunguu Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja
Baadhi
ya Viongozi na Wananchi waliohudhuria katika Baraza la Idi-El-Hajji
lililofanyika huko Tunguu Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein
ameendelea kusisitiza hali ya Amani na kukemea Vitendo vinavyofanywa na
baadhi ya Watu wachache wenye lengo la kuiharibu sifa ya Zanzibar.
Amesema
tangu Karne zilizopita Zanzibar pamekuwa pahala pa Amani na utulivu na
hivyo kuitaka jamii kutoa ushirikiano wa hali ya juu kwa vyombo vya
ulinzi na usalama ili kuwafichua watu ambao wanaoharibu Amani iliyopo.
Rais
Shein ameyasema hayo leo katika Hotuba yake aliyoitoa katika Baraza la
Idd lililofanyika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema
kiujumla hali ya Amani na Utulivu imetanda kote katika Visiwa vya
Zanzibar hali inayopelekea Serikali kupanga na kutekeleza mipango yake
ya kimaendeleo kwa lengo la kuimarisha uchumi na ustawi wa Wananchi
wake.
Hata
hivyo amekea tabia inayofanywa na baadhi ya Watu wachache wanaowahujumu
na kuwatia hofu Wananchi pamoja na Wageni wanaoitembelea Zanzibar.
Amefahamisha
kuwa hakuna Dini inayowaelekeza waumini wake kuwahujumu Wanadamu
wengine na kwamba watakaobainika kufanya vitendo hivyo watachukuliwa
hatua kali za kisheria.
Amewahahakikishia
Wananchi na Wageni kwamba vyombo vya Ulinzi na usalama vinafanya kazi
nzuri ya kusimamia ulinzi na Usalama na kuitaka jamii kutoa ushirikiano
unaohitajika.
Aidha
Dkt. Shein amebainisha kuwa kutokana na kuimarika kwa hali ya usalama
na amani Uchumi wa Zanzibar unaendelea kukua kwa kiwango cha kuridhisha
kutoka Asilimia 6.7 kwa mwaka 2011 hadi Asilimia 7.0 mwaka 2012.
Ameongeza
kuwa hali hiyo inatoa matumaini makubwa hasa ikizingatiwa kuwa ukuaji
wa uchumi katika Bara la Afrika ni Asilimia 5.3 ambapo kwa upande wa
Ukuaji wa uchumi wa Dunia ni Asilimia 2.9
Kuhusu
Zao la Karafuu Dkt. Shein amesema kuwa Shirika la Biashara la Taifa
ZSTC linatarajia kununua tani 4,016 kwa mwaka 2013 na kuwaomba Wananchi
waendelee kushirikiana na Serikali katika kupambana na watu wanaofanya
Magendo ya Karafuu.
Awali
Akimkaribisha Rais Shein kutoa Hotuba yake Waziri wa Katiba na Sheria
Aboubakar Khamis Bakary alisema Serikali imepanga Sala na Baraza la Idd
katika Siku kuu zote za IDD-EL HAJJ zitakuwa zikifanywa kitaifa katika
Mikoa yote ya Unguja na Pemba ambapo kwa mara hii Swala ya Idd
ilifanyika kijiji cha Marumbi Mkoa wa Kusini Unguja.
alifahamisha
kuwa Serikali imeamua kufanya hivyo ili Wananchi wa Mikoa yote ya
Unguja na Pemba wapate fursa ya kuswali pamoja na Viongozi wao Wakuu wa
Kiserikali lakini kwa upande wa Swala ya IDD EL-FITRI itaendelea
kuswaliwa kitaifa katika Mkoa wa Mjini Magharibi.
Sherehe
ya IDD EL HAJJ inakuja kila mwaka kufuatia kumalizika kwa Ibada ya
Hijja inayofanyika MAKKA Nchini Saudia kwa Waislamu wenye uwezo wa
kufanya Ibada hiyo.
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR 16/01/2013
No comments:
Post a Comment