Rais wa Uganda, Yoweri Museveni
amewataka viongozi wawili waandamizi wa upinzani nchini Uganda kuacha
mapambao ya kisiasa wasiyoweza kushinda na badala yake wajiunge na chama
tawala cha National Resistance Movement-NRM.
Bwana Museveni alimshutumu mpinzani
wake Kizza Besigye na meya wa Kampala, Erias Lukwago kwa kupinga program
za maendeleo za serikali na kutangaza uongo. Alitaka aombwe msamaha na
wapinzani hao wawili.
Lakini wote Besigye na Lukwago
walipuuza wito wa Museveni wakiuita mchezo wa kisiasa wa kutaka kupata
uungaji mkono wa chama tawala katika mji mkuu ambako wapiga kura mara
nyingi hawakiungi mkono chama tawala.
Rais Museveni na chama chake tawala
cha NRM wamekuwa madarakani tangu mwaka 1986. Lakini Lukwago anasema
matamshi ya karibuni ya Museveni ni matokeo ya kile anachosema
kinaonekana ni mgawanyiko katika chama tawala.
Lukwago alisema maafisa wa utawala
mara kwa mara wanakataa kufanya kazi na wapinzani kuhusu wasi wasi wa
umma shutuma ambazo wawakilishi wa chama tawala wanazikanusha hazina
ukweli. Wanaushutumu upinzani kwa kuzorotesha juhudi za serikali za
kuendeleza sheria na kanuni na kuhakikisha amani na uthabiti nchini
humo. Kitu ambacho Lukwago hakubaliani nacho. Chanzo: voaswahili
No comments:
Post a Comment