Waziri wa Mambo ya Nje wa Vatican, Askofu Mkuu Pietro Parolin |
Mjadala wa sasa umeibuliwa na Waziri wa
Mambo ya Nje wa Vatican, Askofu Mkuu Pietro Parolin ambaye aliteuliwa
hivi karibuni kushika wadhifa huo aliposema useja, yaani maisha ya
utumishi ndani ya kanisa bila ndoa siyo imani, bali utamaduni na mazoea.
Akizungumzia kauli hiyo, Msemaji wa
Vatican, Federico Lombardi alisema kauli ya Askofu Parolin haipingani na
mafundisho ya kanisa. Askofu Mkuu Parolin ambaye aliteuliwa karibuni na
Papa Francis kushika wadhifa huo kutoka kwa Kardinali Tarcisio Bertone
amenukuliwa na Gazeti la El Universal la Venezuela, Amerika ya Kati
akieleza kuwa suala hilo linaweza kujadiliwa.