Mkurugenzi
wa Biashara wa klabu ya Sunderland.Bw Gary Hutchinson(wapili
kushoto)akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu
hatua ya mazungumzo waliyofikia na kujenga kituo cha michezo katika
Manispaa ya Ilala ambayo itakuwa chimbuko la kuinua mchezo wa mpira wa
miguu(wakwanza kulia)Mkurugenzi wa Michezo Nchini bw.leonard
tadeo(wapili kulia)Mkurugenzi wa Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania
(TTB) Dk. Aloyce Nzuki(wakwanza kushoto)Mwakilishi wa klabu ya
Sunderland Tanzania,Bw Edmund Hazzad.
Mkurugenzi
wa Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk. Aloyce
Nzuki.akifafanua kuhusu sekta ya Utalii inafanikiwa na kuinua uchumi wa
nchi kupitia michezo Nchini.
Mkurugenzi
wa Biashara wa klabu ya Sunderland.Bw Gary
Hutchinson,(kushoto)akimkabidhi mkurugenzi wa wizara ya michezo
bw.leonard Tadeo.jezi ambao imesainiwa sahihi na wachezaji wa
sunderland.
Mkurugenzi
wa Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk. Aloyce
Nzuki(kulia)akimkabizi Mkurugenzi wa Biashara wa klabu ya Sunderland.Bw
Gary Hutchinson,Tisheti ya Bodi ya Utalii.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali walioudhuria kwenye mkutano huo.
SERIKALI
imesema ipo katika hatua za mwisho za mazungumzo na uongozi wa klabu ya
soka ya Sunderland ya Uingereza ili kuwekeza kwenye maendeleo ya sekta
ya Utalii pamoja na kuinua mchezo wa mpira wa miguu nchini.
Akizungumza
mbele ya waandishi wa habari, Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa
Uwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk. Aloyce Nzuki alisema
lengo la kufanya hivyo ni kutafuta wawekezaji wa kuhakikisha sekta ya
Utalii inafanikiwa na kuinua uchumi wa nchi kupitia michezo.
Alifafanua
kuwa tangu kuanza kwa mazungumzo hayo Tanzania imeanza kunufaika kwa
kuwa na ongezeko la watalii la asilimia 30 hali ambayo inaonekuwa kuwepo
kwa mafanikio yanayohitajika.
Alisema
Uingereza ndio nchi inayoongoza kwa utalii nchini na kwamba uwekezaji
huo unalenga kuinua pato la nchi kwa kuongeza ukuaji wa uchumi na
kupunguza umasikini.
"Vivutio
vya Tanzania vinaoneshwa kupitia Uwanja wa timu hiyo nchini Uingereza
katika michuano ya Ligi Kuu ya huko inayoonekana na mashabiki wengi
duniani na kutoa fursa na hamasa kuja nchini kutembelea vivutio vyetu na
kuongeza uchumi wa nchi," alisema.
Pia
Dk. Nzuki aliushukuru uongozi wa klabu ya Sunderland kwa kuendeleza
ushirikiano katika kuinua utalii wa Tanzania kupitia sekta ya michezo
kitu ambacho kila mdau anasubiri mafanikio hayo kwa hamu kubwa ili
Tanzania ifanye vema katika mashindano ya kimataifa.
Wakati
huo huo Mkurugenzi wa Biashara wa klabu ya Sunderland Gary Hutchinson,
alisema moja ya hatua ya mazungumzo waliyofikia na kujenga kituo cha
michezo katika Manispaa ya Ilala ambayo itakuwa chimbuko la kuinua
mchezo wa mpira wa miguu.
Licha
ya kujenga kituo hicho cha michezo (Academy), watajenga uwanja wa kisasa
wa michezo utakaokuwa moja ya sehemu ya uwekezaji katika sekta ya
michezo itakayoleta maendelea katika nyanja hizo na kufikia mafanikio
kwa ushirikiano na kampuni ya Marekani ya Simbion.
"Tutaanzisha
kituo cha michezo (Academy) katika eneo la Kidongo Chekundu wilayani
Ilala, Dar es Salaam ambayo itasaidia kutangaza utalii kimataifa kupitia
sekta ya michezo na kufikia mafanikio yanayohitajika," alisema.
Mkutano
huo wa waandishi wa habari ulihudhuriwa na baadhi ya viongozi wa
Sunderland pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Michezo ya Wizara ya Habari,
Vijana, Utamduni na Michezo.
No comments:
Post a Comment