Friday, May 01, 2015

SUMATRA KIINI CHA AJALI BARABARANI...!!!

Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta

WAZIRI wa Uchukuzi, Samuel Sitta amesema ajali za barabarani zinachangiwa na uzembe wa taasisi inayosimamia sekta ya usafiri jambo linalogharimu maisha ya watu wasio na hatia, na kuitaka taasisi hiyo kuchukua hatua na kuhakikisha nidhamu inarejea kwenye sekta hiyo.

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) ndiyo yenye dhamana ya kusimamia na udhibiti wa sekta ya usafiri katika nchi kavu na majini.

Sitta aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari wakati Kamati ya Bunge ya Miundombinu ilipokuwa ikizungumza na viongozi wa wizara hiyo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

BAN KI-MOON ASIKITISHWA NA MAPIGANO YEMEN

 Ban Ki-moon
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea tahadhari yake kuhusiana na hatari ya raia kuendelea kupigana, Nchini Yemen. Anasema kuwa zaidi ya watu elfu moja mia tano wameuwawa na wengine laki tatu wametoroka makazi yao, katika kipindi cha majuma sita yaliyopita.

Mashambulizi katika majumba ya raia zikiwemo hosptali na maghala ya vifaa vya misaa ya kibinadamu yamekuwa yakiendelea.
Mapigano Yemen
Kumekuwa na taarifa watu wenye silaha wamekuwa wakiwateka raia katika mitaa ya Aden.
Shirika la Umoja wa mataifa la misaada ya chakula limesema halina jinsi zaidi ya kusitisha mipango yake ya kusambaza misaada kutoka na tatizo la mafuta.

Kwa sasa mapigano makali yanaendelea katika mipaka ya eneo la Yemen na Saudia Arabia. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

MAANDAMANO MAPYA BALTIMORE MAREKANI


Kumetokea maandamano mapya nchini Marekani katika mji wa Baltimore kufuatia kifo cha kijana mweusi Freddie Gray aliyekufa kutokana na majeraha akiwa mikononi mwa polisi. Mamia ya watu wameandamana katika mitaa, wakionyesha ujasiri licha ya hali mbaya ya hewa iliyokuwepo.

Matokeo ya mwanzo ya uchunguzi wa polisi wa jinsi kijana wa miaka ishirini na mitano mwenye asili ya weusi alivyouawa bado hayajawekwa hadharani.

Maandamano Baltimore
 
Mtetezi wa haki za binadamu, Mchungaji Al Sharpton, ameitisha mkutano mjini Baltimore ili kuimarisha uhusiano baina ya polisi na wanajamii. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

YANGA INA MATUMAINI YA USHINDI

 
Kocha mkuu wa Yanga Hans Pluijm.
 
Kocha mkuu wa Yanga, Hans Pluijm amesema wana ari ya kushinda mechi yao ya mwishoni mwa wiki hii dhidi ya Etoile du Sahel licha ya kuwaacha wachezaji wake tegemezi katika msafara wao wa Tunisia.

Yanga imeondoka Dar es Salaam Jumatano usiku huku wachezaji wake tegemezi, wakiwemo Hassan Dilunga, Salum Telela na Danny Mrwanda, aliyekuwa akicheza soka la kulipwa nchini Vietnam wakiachwa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kifamilia. “Yanga imesajili zaidi ya wachezaji 20, wote ni muhimu katika timu”.

“Ni kweli niliwahitaji katika mechi yetu ngumu dhidi ya Etoile, lakini sababu mbalimbali zimepelekea kuachwa kwao”, amesema Pluijm. Yanga itacheza na wenyeji wao, Etoile du Sahel katika mechi ya marudiano ya raundi ya 16 bora ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

Katika mechi iliyochezwa wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam, Yanga ililazimishwa sare ya 1-1 hivyo kuwa na kibarua kigumu cha kushinda ugenini huku wenyeji wao wakililia sare ili kucheza hatua inayofuata. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

TAZAMA PICHA ZA YANGA WAKIWA KATIKA MAZOEZI NCHINI TUNIS

IMG-20150501-WA0002
Katika mazoezi ya jana usiku kocha mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amewaambia vijana wake kujiamini na kucheza soka la kushambulia ili kufunga magoli ya mapema  na kuwachanganya Etoile du Sahel katika mechi ya leo usiku kuanzia majira ya saa 3:00 usiku kwa saa za Tanzania.
Mkuu wa Idara ya habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro naye kama kawaida yupo Tunisia kufuatilia mambo yanavyokwenda. Yanga wanahitaji ushindi au sare ya angalau magoli 2-2 ili kusonga mbele moja kwa moja kwasababu mechi ya kwanza jijini Dar es salaam timu hizi zilitoka sare ya 1-1.
Maelekezo ya hapa na pale kabla ya kuanza mazoezi.
Mrisho Ngassa (kushoto) na Simon Msuva (kulia) wanatarajia kuongoza safu ya ushambuliaji leo
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

BEN DAVIES APASULIWA BEGA

 
timu ya Wales 
 
Beki wa kulia wa Tottenham Ben Davies ameenguliwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Wales baada ya kufanyiwa upasuji wa bega. Mlinzi huyu aliumia wakati wa mchezo wa ligi kati ya timu yake na Southampton uliofanyika wiki iliyopita.

Davies hatojumuika na wenzake katika mchezo wa kuwania kuzufu kwa michuno ya ulaya ya mwaka2016. Ambapo Wales watakua na mchezo dhidi ya Ubelgiji , tayari kocha wa timu hiyo Chriss Coleman amemuita kikosini beki wa Swansea City's Neil Taylor kuziba pengo hilo.

Hii inasababisha mchezaji huyu kukosa michezo iliyobaki ya ligi ya England. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Thursday, April 30, 2015

MWANAFUNZI AUAWA BAADA YA KUKUTWA NA BARUA YA MAPENZI

        Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa , Jacob Mwaruanda
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda

MWANAFUNZI wa Kidato cha Pili, Jofrey Robert Mwakatenya (15) anatuhumiwa kuuawa kikatili na baba yake mzazi, Robert Mwakatenya (35) baada ya kumkuta akiwa na barua ya mapenzi, inayodaiwa aliandikiwa na rafiki wake wa kike.

Mzazi huyo ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa eneo la Majengo ‘D’ Manispaa ya Sumbawanga, anadaiwa kumwadhibu mwanafunzi huyo, ambaye ni mtoto wake wa kwanza kwa kupiga ngumi na mateke mfululizo kwa zaidi ya saa tatu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa , Jacob Mwaruanda alithibitisha tukio hilo, lilitokea usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita. Alisema bado wanamtafuta mtuhumiwa huyo kwani baada ya kufanya kitendo hicho alitokomea. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SARAFU YA SH. 500 YATENGENEZEWA MIKUFU

miatano
Sarafu mpya ya shilingi 500


SARAFU mpya ya shilingi 500 inadaiwa kuhujumiwa na baadhi ya watu ambao huinunua kwa Sh 2,500 na baadaye kuiyeyusha kwa ajili ya kutengenezea mikufu ya fedha (silver).

Taarifa ambazo MTANZANIA imezipata kutoka vyanzo mbalimbali zinaeleza tangu sarafu hizo zilipotolewa kwa mara ya kwanza Oktoba mwaka jana, baadhi ya watu wamekuwa wakizikusanya na kuzifanya kuadimika mtaani.


Imeelezwa kuwa tangu kutolewa kwa sarafu hiyo imekuwa adimu mitaani jambo ambalo si kawaida kwa fedha mpya zinazoingizwa kwenye mzunguko kuadimika kwa kiwango hicho. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

'TUTAWAREJESHEA WANANCHI MAJIMBO TATA' DL SLAA

http://jambotz8.blogspot.com/
Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk Willibrod Slaa

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amesema endapo vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vitashindwa kuafikiana katika kuachiana baadhi ya majimbo kabla ya Uchaguzi Mkuu, watawaeleza wananchi kwa kuwa ndiyo kiini cha kuanzishwa kwa umoja huo.

Dk Slaa alisema hayo jana kabla ya kumalizika kwa vikao vya wakuu wa Ukawa ambao wamekubaliana kusimamisha mgombea mmoja kuanzia ngazi ya urais, ubunge na udiwani na kwa siku mbili kuanzia juzi, walikuwa wakijadili ufanikishwaji wa azimio hilo.
Dk Slaa alisema hadi sasa wameshakubaliana kuachiana asilimia 95 ya majimbo yote na kwamba ana matumaini watafanikisha, lakini akaonya kuwa ikishindikana, hawatasita kuwaeleza wananchi. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

ALI KIBA, DIAMOND, JUX WAPETA TUZO ZA KILI

alikiba1
Ali Kiba


WASANII wa muziki wa bongo fleva, Ali Kiba, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Juma Jux, wameingia katika vinyang’anyiro sita vinavyogombewa katika tuzo za muziki ‘Kili Music Award’.
Ali Kiba ameingia kwenye kipengele cha mtumbuizaji bora wa muziki wa kiume, wimbo bora wa mwaka, mwimbaji bora wa kiume, mtunzi bora, video bora ya mwaka na mwimbaji bora wa Afro-Pop.

jux
Juma Jux

 
Naye Diamond ameingia kwenye kipengele cha mtumbuizaji bora, mwimbaji bora, mtunzi bora, wimbo bora wa Zouk, wimbo bora wa Afro Pop na Video Bora ya mwaka kupitia wimbo wa ‘Nitampata Wapi’ na ‘Mdogo Mdogo’.
Diamond
Nasibu Abdul ‘Diamond’

Pia Juma Jux naye ameingia kwenye kipengele cha mwimbaji bora wa kiume, wimbo bora wa mwaka, mtunzi bora wa mwaka, mwimbaji bora wa kiume na wimbo bora wa R&B kupitia nyimbo zake mbili za ‘Sisikii’ na ‘Nitasubiri’.


Mkuu wa matukio wa Baraza la Sanaa Tanzania Basata, Kurwijira Maregesi, alisema zoezi rasmi la upigwaji wa kura litaanza Mei 4 na kufungwa Juni 5 mwaka huu kwa udhamini mkubwa wa Kampuni ya TBL, kupitia bia yake ya Kilimanjaro. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

'SITAVAA NGUO ZA UTUPU TENA' SNURA MAJANGA

snura
Snura Mushi ‘Majanga’


MWIGIZAJI na mwimbaji wa muziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi ‘Majanga’, amesema hatavaa tena nguo za nusu uchi kwa kuwa ameshagundua makosa hayo.

Snura alisema awali alikuwa akivaa mavazi ya nusu uchi au nguo za kumbana, lakini kwa sasa amejirekebisha na anatambua nguo zinazompendeza ili kutokuleta sintofahamu kwa mashabiki wake.


“Kiukweli nashukuru ushauri wa watu katika suala la mavazi, nimeshajirekebisha kwa sasa sivai kama zamani mavazi yasiyofaa katika jamii,” alieleza Snura. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

UGAIDI GARISSA, VYOMBO VYA USALAMA VILIZEMBEA

Watu 150 walipoteza maisha kwenye shambulio la Garissa
Waziri wa usalama wa ndani nchini Kenya Generali Joseph Nkaiserry amekiri kwamba vyanzo na duru za kijasusi zilitahadharisha lakini zilipuuzwa kabla ya shambulizi la Al Shabaab katika chuo kikuu cha Garrissa.

Karibu watu 150 walikufa wakati wa shambulio hilo. Waziri Nkaissery ameongeza kusema shughuli za wokozi zilizofuata pia zilifanywa kiholela.

Baadhi ya Maafisa wakuu wa polisi wamesimamishwa kazi kufuatia shambulia hilo la Chuo Kikuu cha Garrissa. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Na BBC Swahili

KIJANA MDOGO AOKOLEWA AKIWA HAI SIKU BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI...!!!

Kijana aokolewa siku tano baada ya kufunikwa na kifusi
Watoa huduma za uokoaji huko mji mkuu wa Nepal Kathmandu, wamefanikiwa kumuokoa kijana mmoja mwenye umri wa miaka 15 aliyepatikana hai baada ya funikwa na vifusi vya jengo alilokuwemo wakati wa tetemeko la ardhi kukumba taifa hilo siku tano zilizopita.

Licha ya kuwa chini ya maporomoko hayo kwa siku hizo tano isaidiwa na mwanya uliokuwa ukipenyeza hewa iliyomwezesha kupumua japo kwa shida. Makundi ya watu walimshangilia alipotolewa huku akionekana akijitahidi kufungua macho yake.Alikimbizwa hospitali mara moja kupata matibabu zaidi.

Zaidi ya watu 5,500 wamethibitishwa kufariki kutokana na janga hilo. Wengi wa wanavijiji wangali wanasubiri misaada ya chakula na maji safi ya kunywa huku mashirika ya kutoa misaada ya kisema huenda ikachukua siku nyengine 5 kabla ya kuwafikia baadhi yao kutokana na kuharibiwa kabisa kwa miundo mbinu.

Umoja wa mataifa umetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuendelea kutoa misaada wakikadiria michango inayohitajika kuwa zaidi ya dolla millioni 415 kuisaidia Nepal katika kipindi cha miezi 3 ijayo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Thursday, April 23, 2015

AJARI ZARUDI TENA, BASI LAUA 10 SHINYANGA

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga.

Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga
SIKU sita tangu ajali ya basi dogo aina ya Toyota Hiace kuua watu 19 mkoani Mbeya, nchi imeendelea kukumbwa na ajali za barabarani. Safari hii watu kumi wamekatishwa uhai, kutokana na ajali ya basi na lori, iliyotokea mkoani Shinyanga jana.


Katika ajali hiyo, watu tisa walikufa papo hapo na mmoja aliaga dunia akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga. Abiria 51 walijeruhiwa na wanatibiwa hospitali hapo, wakati tisa, akiwemo dereva wa basi, wako katika hali mbaya.

Ajali hiyo ilitokea katika kijiji cha Ibingo Kata ya Samuye wilayani Shinyanga Vijijini na ilithibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha.

Alisema ajali ilitokea majira ya saa 9:30 alasiri baada ya basi la kampuni ya Unique, lililokuwa linatoka Mwanza kwenda Tabora kugongana na lori la kampuni ya Coca Cola, lililokuwa linatoka Kahama. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

ORODHA VYAMA VYA KIJAMII VITAKAVYOFUTWA KUANZA KUTOLEWA

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nch, Isaac Nantanga.
 
WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakati wowote wiki hii itaanza kutoa orodha ya vyama vya kijamii vitakavyofutwa kwa kuanzia na mkoa wa Dar es Salaam.

Imesema vyama hivyo vitafutwa kutokana na kutotekeleza matakwa ya kisheria ya kuwasilisha taarifa za mwaka za ukaguzi wa hesabu za vyama na vile ambavyo havilipi ada ya mwaka kama sheria inavyoelekeza.

Msemaji wa wizara hiyo, Isaac Nantanga alisema hayo jana katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kufafanua suala la uhakiki wa vyama vya kijamii nchini.

Alisema vyama vitakavyobainika vitafutwa katika Daftari la msajili wa vyama vya kijamii na wala siyo Taasisi zisizo za kiserikali (NGO,s) kwani haihusiki nazo.

“Orodha ya vyama vitakavyofutwa itaanza kutolewa kwa awamu kuanzia wiki hii na kwa kuanzia orodha hiyo itahusu vyama vilivyosajiliwa mkoa wa Dar es Salaam”Alisema 

Alisema kufuatana na orodha iliyopo vyama 10,000 vya kijamii na Taasisi za Dini vimesajiliwa na wizara hiyo na vitakavyofutwa ni vile tu ambavyo haviwasilishi taarifa za kila mwaka za ukaguzi wa hesabu zao na pia kama havilipi ada ya kila mwaka kama sheria inavyotaka.

Juzi, gazeti moja la kila siku liliandika kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mathias Chikawe anaanza kuhakiki NGOs jambo ambalo siyo la kweli kinachofanyika ni kwa taasisi za kijamii. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...