Katibu
mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea tahadhari yake kuhusiana
na hatari ya raia kuendelea kupigana, Nchini Yemen. Anasema kuwa
zaidi ya watu elfu moja mia tano wameuwawa na wengine laki tatu
wametoroka makazi yao, katika kipindi cha majuma sita yaliyopita.
Mashambulizi katika majumba ya raia zikiwemo hosptali na maghala ya vifaa vya misaa ya kibinadamu yamekuwa yakiendelea.
Kumekuwa na taarifa watu wenye silaha wamekuwa wakiwateka raia katika mitaa ya Aden.
Shirika
la Umoja wa mataifa la misaada ya chakula limesema halina jinsi zaidi
ya kusitisha mipango yake ya kusambaza misaada kutoka na tatizo la
mafuta.
Kwa sasa mapigano makali yanaendelea katika mipaka ya eneo la Yemen na Saudia Arabia. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment