Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta
WAZIRI wa Uchukuzi, Samuel Sitta amesema ajali za barabarani
zinachangiwa na uzembe wa taasisi inayosimamia sekta ya usafiri jambo
linalogharimu maisha ya watu wasio na hatia, na kuitaka taasisi hiyo
kuchukua hatua na kuhakikisha nidhamu inarejea kwenye sekta hiyo.
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) ndiyo
yenye dhamana ya kusimamia na udhibiti wa sekta ya usafiri katika nchi
kavu na majini.
Sitta aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipozungumza na
waandishi wa habari wakati Kamati ya Bunge ya Miundombinu ilipokuwa
ikizungumza na viongozi wa wizara hiyo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Sitta alisema “Hakuna kitu kinachoniuma kama ajali za barabarani
ambazo nyingi zinasababishwa na uzembe, ubovu wa magari na matairi ya
mtumba, halafu baya zaidi ni kwamba Mamlaka husika ya kudhibiti vyombo
hivyo ipo, inaona na kuwasamehe makosa,” alisema Sitta.
Aliongeza, mamlaka husika zina wajibu wa kusimamia vyombo hivyo na
kuhakikisha vile vinavyofanya makosa vinachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja
na kuvifutia leseni, kwani matukio mengi ya ajali yanatokana na uzembe
na kuanzia sasa masuala ya msamaha yasiwepo.
“Hatuwezi kuendelea kuona wananchi wanakufa tu, kwa sababu ya uzembe
wa madereva au wamiliki, nilizungumza na baadhi ya wamiliki wanasema
hawawezi kununua matairi mapya, kwa sababu ya gharama, wanatumia matairi
ya mtumba, sasa jambo hili sio sahihi, kama hawawezi kutoa huduma kwa
kutumia vyombo vyenye viwango, waache, na sio kucheza na uhai wa watu,”
alisisitiza Sitta.
Sitta aliongeza, wamiliki wa vyombo vya moto na madereva, wanapaswa
kufuata sheria za barabarani na kuhakikisha wanazitii na kwamba vyombo
hivyo vinapaswa kuwa na vipuri vyenye viwango na kuhakikisha mabasi
yanayokwenda umbali zaidi ya kilometa 700, yawe na madereva wawili.
“Ipo sheria inayozungumzia umbali unaotakiwa dereva mmoja aendeshe
gari, lakini pia nilizungumza na daktari kuhusu umbali unaokubalika kwa
madereva kuendesha chombo cha moto, aliniambia dereva mmoja hatakiwi
kuendesha gari kwa umbali wa zaidi ya kilometa 700, zaidi ya hapo
inabidi wawe madereva wawili,” alisema Sitta.
Alisema hiyo inatokana na ukweli kwamba kwa umbali huo, wa kilometa
700 dereva huwa amechoka na akienda zaidi ya hapo anaweza kusababisha
ajali kwa kuwa akili na mwili vimechoka hivyo hawezi kuwa makini
barabarani.
Akizungumzia ubovu wa mabasi ya abiria na daladala, Sitta alisema
magari yote mabovu, yanapaswa yasiwepo barabarani, kwani kuwepo
kunachangia ajali kwa njia moja au nyingine. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Kuhusu mgomo, Sitta alisema nchi inaongozwa kwa sheria na kwamba sio
kila kitu kinachofanywa na serikali ni masuala ya siasa, hivyo sio
sahihi madereva na wamiliki wa mabasi kugoma kutoa huduma kwa abiria.
‘Huwezi kugoma kutoa huduma kwa abiria, halafu madereva wanatoa amri
kwa serikali eti wanatoa siku kadhaa madai yao yatekelezwe, hii ni nchi
inayoongozwa kwa sheria na sio vitisho, hawana haki ya kufanya hivyo,
wanachotakiwa ni kufuata sheria,” alisema Sitta.
Alisema kama kuna madai ya stahiki za madereva na wamiliki wa vyombo
hivyo, wanapaswa kupeleka madai yao sehemu husika na kwamba tatizo kubwa
linaloonekana kwa watu hao ni usaliti wa wao kwa wao.
Alisema mfumo wa malalamiko upo na kwamba kama waliona uamuzi wa
kushusha nauli sio sahihi, walipaswa kukata rufaa, jambo ambalo
wamelifanya na kusubiri rufani yao ndani ya siku 14.
“Hii nchi inaongozwa na sheria, kama wamiliki waliona uamuzi wa
kushusha nauli sio sahihi walipaswa kukata rufaa, jambo ambalo wamefanya
na wasubiri uamuzi wa rufani yao ndani ya muda huo, na majibu ya rufani
yanaweza kukubaliwa au kukataliwa,” alisema Sitta.
Aprili 15 mwaka huu serikali ilitangaza viwango vipya vya nauli
ambavyo vilitarajiwa kuanza kutumika jana Aprili 30, mwaka huu kwa
kushusha nauli za mabasi ya mikoani huku nauli za daladala zikibaki
palepale. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment