Kiungo wa Yanga, Salum Telela, akimiliki mpira mbele ya
wachezaji wa Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara
uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. Yanga imeshinda 8-0.
(Picha na Francis Dande).
Simon Msuva akishangilia bao aliloifungia timu yake.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia.Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
CRISTIANO RONALDO, jana alifunga goli katika ushindi wa magoli 2-0 wa Real Madrid dhidi ya Rayo Vallecano.
Kwa kufunga kwake jana, mchezaji huyo amefikisha magoli 300 tokea
aanze kuichezea Real Madrid, na amekuwa mchezaji wa tatu kwenye historia
ya timu hiyo kufikisha idadi hiyo ya magoli baada ya wakongwe
waliomtangulia kina Alfredo Di Stefano na Raul Gonzalez.
Sasa Cristiano bado magoli manane amfikie Di Stefano na 23 amfikie Raul.
Raul ndie mfungaji bora wa kihistoria kwenye timu hiyo akiwa amefunga
magoli 323 katika mechi 741, wakati marehemu Di Stefano anashika nafasi
ya pili akiwa amefunga magoli 308 katika mechi 396.
Cristiano Ronaldo amefunga magoli 300 katika mechi 288. Hivyo wastani
wake ni mzuri kuliko wachezaji hao wote wawili akiwa na wastani wa
kufunga goli moja katika kila mechi na amefunga magoli mengi kuliko
idadi ya jumla ya mechi alizocheza.
Di Stefano naye wastani wake ni mzuri kuliko Raul. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Ratiba
ya michuano ya kuwania kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika imetolewa
leo na CAF huku Tanzania ikiwa kundi G pamoja na nchi za Nigeria, Misri
na Chad.
Makundi ni kama ifuatavyo:
Kundi A: Tunisia, Togo, Liberia, Djibouti. Kundi B: Congo DRC, Angola, Jamhuri ya Kati, Madagascar. Kundi C: Mali, Guinea ya Ikweta, Benin, Sudan Kusini. Kundi D: Burkina Faso, Uganda, Botswana, Comoro. Kundi E: Zambia, Kenya, Congo Brazzaville, Guinea Bissau. Kundi F: Cape Verde, Morocco, Libya, Sao Tome. Kundi H: Ghana, Msumbiji, Rwanda, Mauritius. Kundi I: Ivory Coast, Sudan, Sierra Leone, Gabon. Kundi J: Algeria, Ethiopia, Lesotho, Shelisheli. Kundi K: Senegal, Niger, Namibia, Burundi. Kundi L. Guinea, Malawi, Zimbabwe, Swaziland. Kundi M. Cameroon, Afrika ya Kusini, Gambia, Mauritania.
Fainali zake zitafanyika Gabon 2017 na droo imefanyika Misri, makao makuu ya CAF. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba juzi
alijikuta akitamka kuwa anakusudia kufuta maadhimisho mbalimbali ya
kitaifa yanayotumika kama kichaka cha kutafuna fedha za Serikali baada
ya wabunge wa upinzani kuitoa jasho Serikali wakati wa kupitisha
Muswada wa Sheria ya Baraza la Vijana wa mwaka 2015.
Mwigulu alitoa kauli hiyo pale alipoingilia kati
mjadala huo, akiponda kitendo cha watumishi wa Serikali kutumia magari
na fedha lukuki katika wiki za kuadhimisha kumbukumbu mbalimbali za
kitaifa.
Kilichoibua mjadala huo ni suala la uanzishwaji wa
Mfuko wa Vijana na maadhimisho ya wiki ya vijana ambayo imepangwa
Oktoba kila mwaka. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Mwonekano wa ndani ya treni ya kisasa ya abiria ya Kampuni ya TRL
iliyozinduliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Shabaan
Mwinjaka, Dar es Salaam jana.
Treni ya kisasa
(Delux), kwenda Bara yenye mabehewa 22 ilianza safari yake ya saa 30
kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma ikiwa ni tofauti ya saa sita
ikilinganishwa na safari ya treni ya zamani.
Kutokana na tofauti hiyo, abiria walioanza safari
kwa furaha na matumaini jana saa tano asubuhi wanatarajiwa kufika Kigoma
leo saa 11 jioni badala ya saa tano usiku.
Hata hivyo, abiria hao watalazimika kuingiza
mikono yao zaidi mifukoni, kutokana na kiwango kipya cha nauli kuwa
Sh79,400 badala ya Sh75,700 za awali kwa daraja la kwanza. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Mashirika ya umoja wa mataifa
yamesema kuwa mamia ya raia wa Yemen wamevuka ghuba ya Aden kwa kutumia
boti ndogo na kuingia nchini Somalia, Djibouti na Somaliland wakikimbia
mapigano nchini mwao.
Shirika la umoja wa mataifa la UNHCR limesema kuwa
linaangalia eneo zuri kwaajili ya kuweka kambi ya wakimbizi kwaajili ya
raia hao. Wakati huo huo wakimbizi kutoka nchini Somalia bado
wanaendelea kuingia nchini Yemen kuepuka njaa na machafuko nchini mwao.
Shirika hilo la UNHCR linasema kuwa Yemen inawahifadhi wakimbizi wapatao
238,000 kutoka Somalia. Mwandishi wa BBC Africa Mary Harper anasema
wazo la Yemen kufikiria kuwa na kambi za wakimbizi nchini Somalia si la
kawaida kwa kuwa ni kawaida kwa raia nchini humo kuikimbia nchi yao
kutokana na machafuko ya mara kwa mara hali ambayo haiwezi kuwa eneo
zuri kwa wakimbizi kuhifadhiwa. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Rais
mteule wa Nigeria, Muhammadu Buhari, amezitaja vurugu zinazosababishwa
na kundi la wanamgambo wa Kiislamu wa Boko Haram kuwa ni tatizo kubwa
linalokabili nchi.
Katika mahojiano maalumu na BBC, kiongozi huyo
mstaafu wa jeshi amesema anatarajia kulishinda kundi hilo baada ya
dhamira mpya kutoka jeshini na msaada wa nchi jirani.
"Kwa ushirikiano
na majirani zetu Cameroon, Chad, Niger na jumuia ya kimataifa na dhamira
ambayo tutapata kutoka katika jeshi, Nafikiri itachukua muda mfupi
zaidi kukabiliana nao."
Jenerali Buhari amesema tayari ameainisha
msingi wa tatizo linalokabili nchi ya Nigeria, lakini amewataka raia wa
nchi hiyo kuwa wavumilivu.
"Tumebaini matatizo makubwa matatu.
Ambayo ni kukosekana kwa usalama nchini, tatizo ambalo kila mmoja
analifahamu na lingine ni ukosefu wa ajira, hii ina maana uharibifu wa
uchumi ikiwa ni kutokana na vitendo vya rushwa na rushwa yenyewe.
Matatizo haya matatu makuu, Wanigeria wote wanafahamu na tunaomba
ushirikiano wa wananchi wa Nigeria, wasitarajie miujiza kutokea katika
kuyapatia ufumbuzi matatizo haya katika kipindi cha miezi michache baada
ya kutwaa madaraka kwa sababu uharibifu umechukua miaka mingi, miaka
kumi na sita ya utawala wa chama tawala cha nchi hii."
Anasema rais huyo
mteule wa Nigeria. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limemtaka Mchungaji
Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, kujisalimisha
polisi kwa tuhuma za kumkashifu Kiongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar
es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Hatua hiyo ya polisi imekuja baada ya jeshi hilo kupokea malalamiko,
ambapo inadaiwa Mchungaji Gwajima alitoa lugha ya kashfa dhidi ya
Kardinali Pengo ambaye alipinga tamko lililotolewa na Jumuiya ya
Kikristo Tanzania (CCT) la kuipigia kura ya Hapana Katiba
Inayopendekezwa.
Taarifa iliyotolewa jana na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es
Salaam na Kamanda wa Polisi, Kamishna Suleiman Kova, imemtaka Mchungaji
Gwajima kujisalimisha haraka katika Kituo cha Polisi cha Kati kwenye
Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda kwa mahojiano kuhusu tuhuma za kashfa
na matusi.
RAIS Jakaya Kikwete amewateua Dk. Grace Puja na Innocent Sebba kuwa wabunge wapya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Taarifa iliyotolewa jijini Dar es Salaam jana na Mwandishi Msaidizi wa
Rais, Premi Kibanga, ilisema uteuzi huo unatokana na mamlaka aliyopewa
rais na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 66 (I) (e).
Alisema ibara hiyo, inampa mamlaka rais ya kuteua wabunge wasiozidi 10
na kwamba uteuzi wa wabunge hao ulianza Machi 20, mwaka huu. Kibanga alisema kuteuliwa kwao kumekamilisha idadi ya wabunge ambao rais amepewa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo kikatiba.
Alisema awali Rais Kikwete aliwateua Profesa Makame Mnyaa Mbarawa ambaye
ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dk. Asha Rose Migiro
(Waziri wa Katiba na Sheria), Saada Salum Mkuya (Waziri wa Fedha) na
Janeth Mbene (Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara).
Wengine walioteuliwa awali ni Profesa Sospeter Muhongo, Shamsi Vuai
Nahodha, Zakhia Meghji na Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR-Mageuzi, James
Mbatia. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Utafiti mpya
umebaini kuwa wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro wanaongoza kwa unywaji wa
pombe hasa ya viroba, ikiwa ni mara nne zaidi ya wakazi wanaokunywa
pombe katika mikoa ya Mwanza na Geita.
Katika utafiti huo uliofanywa na Taasisi ya Taifa
ya Utafiri wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kupitia mradi wa Strive
ulibaini kuwa idadi kubwa ya wanaokunywa pombe ni vijana wenye umri wa
kati ya miaka 15 hadi 24.
Utafiti huo wa NIMR ulilenga kujua ukubwa wa
Matumizi ya Pombe kwa vijana katika mikoa ya Kilimanjaro, Mwanza,
Geita na Kahama umebaini kuwa mkoa wa Kilimanjaro unaongoza kwa unywaji
wa pombe kwa vijana wenye umri kutokana na utamaduni uliopo mkoa huo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
BOSI wa kundi la Young Money, Lil Wayne, amemuweka wazi mpenzi wake
mpya, Christina Milian, ambaye ni mmoja wa wanachama wa kundi hilo
analoliongoza.
Baada ya kuweka wazi habari hiyo, Wayne kupitia mtandao wa Twitter,
aliandika, “Samahani kwa kusubiri muda mrefu kujua nini kinaendelea, kwa
sasa hakuna tena maswali nikiwa na Christina, huyu ni mpenzi wangu.”
Wayne ni baba wa watoto watano, na sasa yeye, mpenzi wake huyo na mtoto
wake wa kwanza, Regina aliyezaa na mama mwingine wanafanya kazi pamoja
katika kundi hilo.
SIKU moja baada ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kumuonya aliyekuwa
Waziri Mkuu Edward Lowassa, kwa tuhuma za kukiuka Katiba na kuanza
kampeni za Urais kabla ya muda, kiongozi huyo ameibuka na kudai kuwa
hana njia ya kuwazuia watu wasimuombe agombee Urais.
Pia Lowassa ametumia nafasi hiyo na kuwaomba wale wote ambao bado
wana nia ya kumshawishi agombee nafasi hiyo ya urais, wasubiri kwanza
hadi pale chama chake hicho kitakapotoa maelekezo.
Akizungumza na vijana 60 wa bodaboda kutoka wilaya ya Mbarali, Mbeya
waliokwenda pia kumshawishi agombee nafasi hiyo, mjini Dodoma jana,
alisema si vyema kwa maofisa wa chama kuzungumzia masuala ya wanachama
wao kwenye vyombo vya habari wakati kuna vikao vya chama.
Alisema watu waliojitokeza na kumshawishi kuchukua fomu za kuwania
nafasi hiyo ya Urais, hajawaita wala kuwalipa chochote kama inavyodaiwa
na kwamba walikuwa wakifuata maneno ya Rais Jakaya Kikwete aliyoyatoa
mkoani Ruvuma katika sherehe za maadhimisho ya miaka 38 ya Uhuru.
Alisema katika siku hiyo, Rais Kikwete aliwataka watanzania
wawashawishi viongozi wanaoona wanafaa ili wajitokeze kugombea nafasi
hiyo ya Urais. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.