Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba juzi
alijikuta akitamka kuwa anakusudia kufuta maadhimisho mbalimbali ya
kitaifa yanayotumika kama kichaka cha kutafuna fedha za Serikali baada
ya wabunge wa upinzani kuitoa jasho Serikali wakati wa kupitisha
Muswada wa Sheria ya Baraza la Vijana wa mwaka 2015.
Mwigulu alitoa kauli hiyo pale alipoingilia kati
mjadala huo, akiponda kitendo cha watumishi wa Serikali kutumia magari
na fedha lukuki katika wiki za kuadhimisha kumbukumbu mbalimbali za
kitaifa.
Kilichoibua mjadala huo ni suala la uanzishwaji wa
Mfuko wa Vijana na maadhimisho ya wiki ya vijana ambayo imepangwa
Oktoba kila mwaka. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
“Napendekeza wiki hii (ya Mfuko wa Vijana)
iondolewe mwezi Oktoba kwa sababu ndani ya wiki hiyo pia kuna
maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Nyerere na kuhitimisha
mbio za mwenge,” alisema Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika.
Kauli ya Mnyika iliungwa mkono na Mbunge wa
Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyesema si jambo la busara
kuiweka siku hiyo sawa na kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Nyerere.
“Kila mtu hapa anajua jinsi siku ya kilele cha mwenge yanavyofanyika mambo mabaya. Hatulitaki jambo hili,” alisema Lissu.
Msimamo huo ulimnyanyua Naibu Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia na kusema kuwa hata Mwalimu
Nyerere alikuwa kijana wakati akifanya harakati za kulikomboa Taifa, si
vibaya kama Wiki ya Vijana ikaadhimishwa mwezi huo.
Kwa nyakati tofauti Mawaziri Jenister Mhagama,
Mary Nagu, Dk Fenella Mukangara na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George
Masaju walisimama kuitetea hoja hiyo bila mafanikio.
Wakati mvutano ukizidi kuwa mkali, alisimama
Mwigulu na kusema: “Mimi nina mawazo tofauti kidogo. Nadhani umefikia
wakati wa kufikiri tofauti na kuachana na hizi kumbukumbu za wiki ya
maafa, wiki ya mtoto wa jicho, wiki ya kichaa cha mbwa, wiki ya maziwa,
sijui kunyonyesha… sijui wiki ya nini. Nikiwa...”(akakatishwa na
Mwenyekiti wa Bunge Zungu).
Mwigulu alisema katika maadhimisho hayo watumishi
wa Serikali hutumia mamilioni ya fedha na magari ya Serikali kushiriki,
kuifanya Serikali kutumia fedha nyingi katika mambo ambayo si ya msingi
sana.
“Kuna maadhimisho Mtwara watendaji kutoka Mwanza
wanakwenda. Sijui kuna shughuli Kigoma watu wanatoka Dar es Salaam.
Tufikie wakati tuachane na hizi wiki na tubaki na maadhimisho ya
muhimu,” alisema. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Akifafanua baadaye jana, Mwigulu alisema,
“Nililenga kuonyesha jinsi fedha zinavyotumika hovyo. Unajua katika
maadhimisho haya, watu wanatengeneza fulana, kofia na mambo mengine
mengi. Sidhani kama ni sahihi.” Alisema kuna mambo mengi ya msingi
yanayohitaji kufanyika lakini fedha zinakosekana, kama maadhimisho ya
wiki yakiangaliwa kwa umakini, fedha nyingi zinaweza kuokolewa.
Alipoulizwa alitaka kusema nini aliposema niki... alisema kuna
kitu alitaka kusema lakini hakumalizia, ingawa hoja yake ilikuwa
kusisitiza kuwa fedha nyingi za Serikali zinatumika vibaya katika
maadhimisho hayo.
Hata hivyo, pamoja na kauli hiyo, Mwigulu
alipohitimisha kauli hiyo bungeni alipondwa na Lissu na Mnyika wakisema
kuwa kauli yake haikutakiwa kutolewa na mtu kama yeye, kwamba licha ya
kuwa ni waziri mdogo, pia anataka kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa
Oktoba mwaka huu.
Mvutano huo haukufikia mwafaka na kumlazimisha
Zungu kulihoji Bunge kama linakubaliana na hoja ya wapinzani. Kutokana
na wingi wa wabunge wa CCM, hoja ya Serikali ya kuanzisha mfuko katika
baraza hilo iliungwa mkono.
Hata hivyo, baadhi ya watu wametafsiri kuwa Mwingulu aliposita na kutamka nikiwa.. alitaka kusema nikiwa Rais. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment