Mwonekano wa ndani ya treni ya kisasa ya abiria ya Kampuni ya TRL iliyozinduliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Shabaan Mwinjaka, Dar es Salaam jana.
Treni ya kisasa
(Delux), kwenda Bara yenye mabehewa 22 ilianza safari yake ya saa 30
kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma ikiwa ni tofauti ya saa sita
ikilinganishwa na safari ya treni ya zamani.
Kutokana na tofauti hiyo, abiria walioanza safari
kwa furaha na matumaini jana saa tano asubuhi wanatarajiwa kufika Kigoma
leo saa 11 jioni badala ya saa tano usiku.
Hata hivyo, abiria hao watalazimika kuingiza
mikono yao zaidi mifukoni, kutokana na kiwango kipya cha nauli kuwa
Sh79,400 badala ya Sh75,700 za awali kwa daraja la kwanza. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Huku nauli za daraja la pili ikishuka kutoka
Sh55,400 hadi Sh,47,600 zile za daraja la tatu zimepanda kutoka Sh27,700
hadi Sh35,700.
Kwa mtazamo wa haraka, mabehewa hayo yanavutia
yakilinganishwa na yale ya awali yaliyokuwa yamekithiri kwa uchakavu,
yaliyokuwa yamejaa mende na yenye milango na madirisha mabovu.
Mabehewa hayo yana viti vya kutosha, huduma ya
intaneti, swichi za umeme za kuchajia simu na kuunganisha kompyuta na
safari zake zimeongezeka kutoka mbili hadi tatu kwa wiki.
Akizungumza muda mfupi kabla uzinduzi huo,
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Mhandisi Kipallo
Kisamfu alisema wamelazimika kupandisha viwango vya nauli kutokana na
gharama zitakazokuwa zinatumika katika uendeshaji wa treni hiyo.
“Licha ya kuongeza kidogo kiwango cha nauli,
dhamira yetu ni kuwapatia abiria huduma safi na ya raha... kila msafiri
atasafiri akiwa ameketi kwenye kiti chake.
Hakuna abiria atakayesafiri akiwa amesimama,” alisema na kuongeza: “Treni inayozinduliwa leo inatumia mabehewa mapya 22 yaliyonunuliwa kutoka Korea Kusini na kichwa cha treni kiliundwa upya kwenye karakana ya TRL iliyopo Morogoro mabehewa mapya yamegharimu Serikali Sh28.6 bilioni.”
Hakuna abiria atakayesafiri akiwa amesimama,” alisema na kuongeza: “Treni inayozinduliwa leo inatumia mabehewa mapya 22 yaliyonunuliwa kutoka Korea Kusini na kichwa cha treni kiliundwa upya kwenye karakana ya TRL iliyopo Morogoro mabehewa mapya yamegharimu Serikali Sh28.6 bilioni.”
Kuhusu vituo vya ambavyo treni hiyo alisema itasimama kwenye vituo vikubwa ambavyo vingi ni vile vya miji, wilaya na mikoa.
Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Dk Shabaan
Mwinjaka aliwataka abiria kuwa walinzi wa treni hiyo ili kuhakikisha
usafiri huo unadumu.
“Kumekuwa na tabia ya watu kujiamulia kuharibu
mali za umma, ninawaomba abiria mtakaopanda treni hii muwe walinzi wa
wenzenu kwa sababu baadhi ya abiria wamekuwa na tabia ya kuchora kwenye
viti,” alisema Dk Mwinjaka.
Mmoja wa abiria, Saida Roman alisema Serikali
inahitaji kupewa pongezi kwa hatua hiyo kwani hivi sasa abiria
wanaotumia usafiri wa treni kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma
watasafiri kwa raha tofauti na ilivyokuwa zamani. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment