Mashirika ya umoja wa mataifa
yamesema kuwa mamia ya raia wa Yemen wamevuka ghuba ya Aden kwa kutumia
boti ndogo na kuingia nchini Somalia, Djibouti na Somaliland wakikimbia
mapigano nchini mwao.
Shirika la umoja wa mataifa la UNHCR limesema kuwa
linaangalia eneo zuri kwaajili ya kuweka kambi ya wakimbizi kwaajili ya
raia hao. Wakati huo huo wakimbizi kutoka nchini Somalia bado
wanaendelea kuingia nchini Yemen kuepuka njaa na machafuko nchini mwao.
Shirika hilo la UNHCR linasema kuwa Yemen inawahifadhi wakimbizi wapatao
238,000 kutoka Somalia. Mwandishi wa BBC Africa Mary Harper anasema
wazo la Yemen kufikiria kuwa na kambi za wakimbizi nchini Somalia si la
kawaida kwa kuwa ni kawaida kwa raia nchini humo kuikimbia nchi yao
kutokana na machafuko ya mara kwa mara hali ambayo haiwezi kuwa eneo
zuri kwa wakimbizi kuhifadhiwa. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment