Viwanda vikitoa moshi angani na kuchafua mazingira
Mwaka
huu unaoishia unasemekana kuwa na kiwango cha juu zaidi cha joto
duniani na kwa Uingereza tangu kumbukumbu zianze kutunzwa.
Makadirio
ya awali yanaonyesha kuwa katika miezi kumi ya kwanza ya mwaka 2014,
wastani wa kiwango cha hali ya joto duniani kilikuwa 0.57C juu ya
wastani uliokuwepo muda mrefu.
Dhoruba nchini Uingereza iliyosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi
Na miezi kumi na mmoja ya
kwanza nchini Uingereza imezalisha wastani wa joto la 1.6C likiwa juu ya
wastani uliokuwepo kwa muda mrefu.Utafiti mwingine uliofanywa na
Ofisi ya Hali ya Hewa ya Uingereza umeonyesha kuwa ongezeko la viwango
vya joto vilivyoshuhudiwa, visingetokea bila ya ongezeko la gesi
zinazoharibu mazingira kutokana na shughuli za binadamu. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza
kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Wapiganaji wa Islamic State katika jimbo la Anbar,Syria Marchi 2014
Wapiganaji wa kundi la Islamic State wafungua kambi za mafunzo Libya
Wapiganaji
wa kundi la Islamic State wameanzisha kambi za mafunzo mashariki mwa
Libya, amesema mkuu wa kamandi ya Marekani ya masuala ya Afrika.
Wapiganaji wa Kikurd wakiwa katika mafunzo ya
kijeshi kukabiliana na wapiganaji wa Islamic State Septemba 2014 nchini
Iraq.Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza
kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Upangaji
wa makundi ya timu kumi na sita zilizofuzu kucheza fainali za
mashindano ya 30 ya kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2015
yamefanyika katika mji mkuu wa Equatorial Guinea, Malabo.
Mashindano hayo yataanza Januari 17, 2015.
Upangaji
wa makundi ulirudishwa wiki moja nyuma ili kuiwezesha Equatorial
Guinea, kujiandaa baada ya kuchukua nafasi ya Morocco, iliyokuwa iandae
mashindano hayo, lakini ilishindwa kufanya hivyo baada ya kutaka
mashindano hayo yasogezwe mbele kuhofia ugonjwa wa Ebola ambao
umeyakumba baadhi ya mataifa ya Afrika Magharibi, ambako zinatoka timu
nyingi zinazoshiriki michuano hiyo.
Mabingwa watetezi Nigeria ni
moja ya timu kubwa zilizoshindwa kufuzu kucheza fainali za mwakani,
pamoja na Misri na Angola ambazo zote kwa mshangao hazitaweza kushiriki.
Haya hapa makundi manne ya AFCON 2015:
Kundi A Equatorial Guinea, Burkina Faso, Gabon, Congo Kundi B Zambia, Tunisia, Cape Verde, DR Congo Kundi C Ghana, Algeria, South Africa, Senegal Kundi D Ivory Coast, Mali, Cameroon, Guinea
Wenyeji
Equatorial Guinea na Congo zitacheza mechi ya ufunguzi wa michuano
hiyo. Kundi D ndilo linaloonekana kuwa gumu zaidi kutokana na timu
zilizopangwa kundi hilo. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza
kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Ivanovic akishangilia na Drogba baada ya Drogba
kuifungia timu yake ya Chelsea bao la pili katika mechi hiyo
Mzunguko wa 14 umekamilika kwa timu zote 20 za ligi kuu ya England kushuka viwanjani.
Chelsea,
wameendeleza wimbi la ushindi na kukataa katakata kuzipa nafasi timu
nyingine 19 kupunguza pengo la pointi lililopo kati yake na timu hizo.
Sergio Aguero, mchezaji wa Manchester City akishangilia moja ya magoli yake katika ligi kuu ya England
Chelsea imeendelea kuwa na
tofauti ya pointi sita na Man City inayoifuatia baada ya kuirarua
Tottenham mabao 3-0, huku Manchester City yenye pointi 30 ikiisasambua
Sunderland magoli 4-1. Sergio Aguero ameifungia timu yake ya Manchester
City magoli mawili katika mchezo huo, huku Jovetic na Zabaleta kila
mmoja akifunga bao moja. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza
kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila. PICHA|MAKTABA
Mbunge wa Kigoma Kusini
(NCCR-Mageuzi), David Kafulila ameeleza namna alivyoibua sakata la
uchotwaji wa Sh306 bilioni kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow na kudokeza
kuwa kitendo cha baadhi ya watuhumiwa kugoma kujiuzulu, kinaonyesha kuna
watu zaidi wanahusika.
Kafulila (32), ambaye alikuwa akiulizia suala hilo
kila mara bungeni hadi uamuzi wa kulijadili ulipofikiwa, amesema
ataendelea kulifuatilia hadi aone mwisho wake.
Akaunti hiyo ilifunguliwa Benki Kuu ya Tanzania
(BoT) kuhifadhi fedha za malipo ya tozo ya ufuaji umeme baada ya Tanesco
kuingia kwenye mgogoro na Kampuni ya IPTL na suala hilo kupelekwa
mahakamani.
Kwa mujibu wa masharti ya uendeshaji wa akaunti za
escrow, fedha hizo zilitakiwa zitolewe baada ya Mahakama kutoa uamuzi
wa mgogoro huo, lakini wakati ilitaka pande hizo mbili zikutane na
kukokotoa viwango vya tozo hizo, fedha hizo zilitolewa na kulipwa kwa
mmiliki mpya wa Kampuni ya Pan African Power Solutions (PAP), jambo
lililosababisha kuibuka kwa kashfa hiyo. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba. PICHA|MAKTABA
Mwenyekiti wa
iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema wizi
wa Sh306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow, mvutano kati ya
mihimili ya dola na viongozi kukosa maadili ni matokeo ya nchi kuwa na
Katiba isiyo na majibu ya masuala hayo.
Akizungumza katika
mahojiano maalumu na gazeti hili, Jaji Warioba alisema Bunge la Katiba
lilifanya makosa kutoviweka vifungu vinavyozungumzia mambo hayo katika
Katiba Inayopendekezwa ambavyo awali vilipendekezwa na Tume yake katika
rasimu ya pili.
“Katika mchakato wa Katiba Mpya tulisema kuwe na
mgawanyo wa madaraka na kila mtu ajue madaraka yake ni nini na
kutenganisha Serikali na Bunge. Kama Serikali na Bunge vingetenganishwa
bungeni usingeibuka mvutano kuhusu waliochota fedha za escrow. Bunge
lingekuwa huru katika utendaji wake wa kazi,” alisema. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Spika wa Bunge la Uganda Bi Rebecca Kadaga awashauri wanaume kutowaoa wanawake waliokeketwa.
Spika
wa Bunge la Uganda Bi Rebecca Kadaga amewashauri wanaume kutowaoa
wanawake waliokeketwa akiwataja kuwa mzigo ambao hauwezi kuijenga jamii.
Kulingana
na gazeti la daily Monitor,Spika Kadaga alitoa wito huo wakati wa
sherehe ya kitamaduni ambayo inapinga ukeketaji ilioandaliwa na mfuko wa
umoja wa mataifa unaosimamia idadi ya watu na wahisani wengine. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Mlipuko mkubwa umetokea katika mji wa Mogadishu nchini Somalia karibu na uwanja wa ndege.
Duru zimearifu kuwa mlipuko huo huenda umesababishwa na mtu aliyejitolea muhanga aliyejilipua ndani ya gari. Kundi
la wapiganaji wa kiislamu la Al- Shaabab mara kwa mara hutumia milipuko
ya magari, lakini kufikia sasa halijakiri kuhusika na mlipuko huo. Haijajulikana ni watu wangapi wameuwawa. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Droo ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015 kufanyika leo usiku mjini Malabo nchini Equitorial Guinea.
Mabingwa
wa zamani Zambia na waandalizi wa kombe la bara Afrika Equitorial
Guinea ni miongoni mwa timu zitakazoorodheshwa katika droo ya kombe hilo
la mwaka 2015 Jumatano usiku.
Shirikisho la soka barani Afrika
CAF tayari limezigawanya timu hizo 16 katika makundi vyungu vinne vya
kinyang'anyiro hicho cha january 17 hadi februari 8. Hatua hio
ilifanyika kulingana na utendaji wa timu hizo katika awamu tatu ya
michuano hiyo na mechi za kufuzu katika kipindi hicho hicho. Miongoni mwa vitu ambavyo vilitiliwa mkazo ni matokeo ya mechi za kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2014. Droo
hiyo ambayo itabuni makundi manne yanayoshirikisha timu moja moja
kutoka kila chungu itafanyika mjini malabo jumatano usiku. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz Ghana
na Ivory Coast ni timu nyengine kubwa huku washindi wa pili wa mwaka
3013 Burkina Faso wameorodheshwa katika kundi la Pili. 2015 Nations Cup :Timu zilivyowekwa. Pot 1: Equatorial Guinea, Ghana, Ivory Coast, Zambia Pot 2: Burkina Faso, Mali, Tunisia, Algeria Pot 3: Cape Verde, South Africa, Cameroon, Gabon Pot 4: Guinea, Senegal, DR Congo, Congo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa Mussa Juma Assad kuwa
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Desemba Mosi,
2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, inasema kuwa uteuzi
wa Bwana Assad ulianza Novemba 5, mwaka huu, 2014.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa Bwana Assad ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 2, saa nne asubuhi, Ikulu, Dar es Salaam. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Nia kuu ya Boko Haram ni kuwa na dola ya kiisilamu inayofuata sheria za kiisilamu.
Watu
wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Boko Haram wamefanya mashambulizi
katika miji miwili eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
La kwanza lilikuwa la kujitoa mhanga pamoja na shambulizi lengine katika kituo cha polisi cha Damaturu. Wenyeji wa mji wa Maiduguri walielezea kusikia milipuko miwili kwenye soko moja. Mashambulizi mengine ya kujitoa mhanga eneo hilo wiki iliyopita yaliwaua zaidi ya watu 70. Mapema
leo Jumatatu watu wanaokisiwa kuwa wanamgambo wa Boko Haram
waliteketeza kituo cha polisi katika mji wa Damataru kilicho umbali wa
kilomita 100 Magharibi mwa mji wa Maiduguri. Inaarifiwa watu 5 wameuawa katika mashambulizi hayo ya mabomu yaliyotokea katika soko lililokuwa na watu wengi. Mjini Damaturu , milipuko na milio ya risasi ilisikika huku wanamgambo hao walipokuwa wanashambulia mjini huo. Boko Haram imeahidi kubuni dola ya kiisilamu katika maeneo ambayo kundi hilo linadhibiti. Milipuko
hio ilitokea Jumatatu katika soko la Maiduguri , mji mkuu wa jimbo la
Borno ambayo ilisababishwa na wasichana wawili waliojilipua. Takriban watu 32 walijeruhiwa katika milipuko hio. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Mahakama ya ICC imetupilia mbali ombi la Lubanga kupunguziwa kifungo jela.
Mahakama
ya kimataifa ya ICC mjini Hague, imetupilia mbali ombi la rufaa
lililowasilishwa na muasi wa zamani nchini DRC Thomas Lubanga dhidi ya
hukumu aliyopewa kwa makosa ya kuwatumia watoto kama wanajeshi.
Viongozi
wa mashtaka walisema wavulana wadogo wenye umri wa miaka 10 walitekwa
nyara na kusajiliwa kama wanajeshi DRC katika vita hivyo vilivyoanza
mwaka 1999. Wasichana nao walitumiwa kama watumwa wa ngono. Mnamo mwaka 2012, Lubanga alikuwa mtu wa kwanza kuhukumiwa na mahakama hio. Aliwahi
kuwa kiongozi wa kundi la wapiganaji la (UPC), ambalo lilikuwa la
kabila la Hema ambalo lilihusika katika vita eneo la Ituri Mashariki mwa
DRC. Mahakama ilimpata na hatia kwa kuwatumia watoto kama wanajeshi na kuwatuma kwenda kumpigania. Alihukumiwa kifungo cha miaka 14. Kundi
la UPC, lilikuwa moja ya makundi sita ya wapiganaji waliopigana
kudhibiti eneo lenye utajiri wa madini la Ituri hadi mwaka 2003. Mgogoro
ulianza kama mvutano wa kupigania mali asili, ingawa baadaye ilipanda
daraja na kuwa vita vilivyohusisha jeshi la Uganda. Kadhalika mgogoro huo uligeuka na kuwa vita kati ya jamii za Hema na Lendu ambapo takriban watu 50,000 waliachwa bila makao. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
MSANII
Naseeb Abdul 'Diamond Platumz' ametwaa tuzo tatu za Channel O usiku wa
kuamlia leo nchini Afrika Kusini. Tuzo hizo ni; Most Gifted new comer,
Most Gifted Afropop na Most Gifted East kupitia wimbo wake wa Number
One! Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz