Wapiganaji wa Islamic State katika jimbo la Anbar,Syria Marchi 2014
Wapiganaji wa kundi la Islamic State wafungua kambi za mafunzo Libya
Wapiganaji
wa kundi la Islamic State wameanzisha kambi za mafunzo mashariki mwa
Libya, amesema mkuu wa kamandi ya Marekani ya masuala ya Afrika.
Wapiganaji wa Kikurd wakiwa katika mafunzo ya
kijeshi kukabiliana na wapiganaji wa Islamic State Septemba 2014 nchini
Iraq.Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza
kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo TzJenerali David Rodriguez
amesema kuna mamia ya wapiganaji wa IS wanaopata mafunzo ya kijeshi
kwenye kambi zake nchini Libya. Amesema kambi hizo zipo katika hatua za
mwanoz kabisa, lakini Marekani imekuwa ikiyafuatilia kwa karibu kuona
zinavyoendelezwa.Libya imekuwa katika mgogoro tangu kuangushwa
kwa utawala wa Muammar Gaddafi mwaka 2011, ambapo makabila mbalimbali,
wanamgambo na makundi ya kisiasa, wote wakipigania madaraka. Makundi
mbalimbali ya Kiislam yanawania madaraka mashariki mwa Libya, huku
baadhi yakitangaza kuwa na ushirikiano la kundi la Islamic State, IS.
Wapiganaji kutoka kikundi cha IS wakipakia
mabaki ya kile kinachosemekana kuwa mabaki ya ndege ya Marekani
isiyotumia abiria baada ya kukonga katika mnara wa mawasiliano huko
Raqqa Septemba 23,2014
Akizungumza mjini Washington
Jumatano, Jenerali Rodriguez bado haijafahamika ukaribu uliopo kati ya
watu wanaopata mafunzo hayo na kundi la IS."Kikubwa ni watu
wanaokuja kupata mafunzo na msaada wa vifaa kwa ajili ya kambi za
mafunzo kwa sasa," amesema. "kwa sasa mafunzo hayo bado ni ya hatua ya
chini sana na tunafuatilia kuona namna hali inavyokwenda."
Watoto wakikimbia kando ya mlima hukumoshi
ukisambaa angani kufuatia mapigano katika eneo hilo la mji wa Kobani,
wakati majeshi yanayoongozwa na Marekani kushambulia wapiganaji wa
Islamic State
Waandishi wa habari wanasema
katika kipindi cha mapinduzi yaliyomwondoa madarakani Gaddafi,
wapiganaji wengi waasi waliondoka nchini humo kwenda kujiunga na vikundi
vya wapiganaji nchini Syria na baadhi yao wanaaminika kuwa wamerejea
nyumbani(Libya).Serikali iliyochaguliwa imepoteza miji mikuu mitatu ya Libya huku kukiwa na mgogoro wa kisiasa. Benghazi,
mji wa pili kwa ukubwa nchini Libya, uko mikononi mwa wapiganaji wa
Kiislam, na bunge linalotambuliwa kimataifa kwa sasa linaendesha vikao
vyake katika mji ulioko pwani ya Tobruk mashariki mwa nchi hiyo. Marekani
imekuwa ikiongoza washirika wa kimataifa kufanya mashambulio ya anga
dhidi ya IS nchini Iraq na Syria katika miezi ya karibuni.
No comments:
Post a Comment