Viwanda vikitoa moshi angani na kuchafua mazingira
Mwaka
huu unaoishia unasemekana kuwa na kiwango cha juu zaidi cha joto
duniani na kwa Uingereza tangu kumbukumbu zianze kutunzwa.
Makadirio
ya awali yanaonyesha kuwa katika miezi kumi ya kwanza ya mwaka 2014,
wastani wa kiwango cha hali ya joto duniani kilikuwa 0.57C juu ya
wastani uliokuwepo muda mrefu.
Dhoruba nchini Uingereza iliyosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi
Na miezi kumi na mmoja ya
kwanza nchini Uingereza imezalisha wastani wa joto la 1.6C likiwa juu ya
wastani uliokuwepo kwa muda mrefu.Utafiti mwingine uliofanywa na
Ofisi ya Hali ya Hewa ya Uingereza umeonyesha kuwa ongezeko la viwango
vya joto vilivyoshuhudiwa, visingetokea bila ya ongezeko la gesi
zinazoharibu mazingira kutokana na shughuli za binadamu. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza
kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Mabadiliko ya tabia nchi yanayochochewa na shughuli za kibinadamu
Shirika la Hali ya Hewa la
Umoja wa Mataifa, WMO, limeonya kuwa dunia inakabiliwa na mwaka wenye
kiwango cha juu kabisa cha joto tangu rekodi zianze kuchukuliwa ambapo
shirika hilo limesema, inathibitisha mwenendo wa ongezeko la joto
likiendana na mabadiliko ya tabia nchi.Shirika hilo limesema
kupanda kwa viwango vya joto katika uso wa bahari vilikuwa vinasababisha
mvua zisizo za kawaida katika nchi za Morocco, Uturuki na nchi za
Blakan, Ulaya mashariki na kusababisha ukame mkali katika maeneo mengine
duniani. Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani, Michel Jarraud,
amesema kuongezeka kwa utoaji wa gesi zinazoharibu mazingira na
mgandamizo wake angani kunaisababishia dunia kutokuwa na uhakika wa hali
ya hewa na hali mbaya ya baadaye. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza
kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment