Rais Jakaya Kikwete akiagana na daktari bingwa, Edward Schaeffer baada
ya kuruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Johns Hopkins, Baltimore nchini
Marekani, alikofanyiwa upasuaji mwishoni mwa wiki iliyopita.
Rais Jakaya Kikwete ametoka
wodini katika Hospitali ya Johns Hopkins na kuhamishiwa kwenye hoteli
maalumu ambako ataendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.
Rais Kikwete alifanyiwa upasuaji wa tezi dume wiki iliyopita na afya yake imekuwa ikiimarika siku hadi siku.
Makundi mbalimbali ya wananchi yamekuwa yakimtakia
uponaji wa haraka kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu. Miongoni mwa
waliomtakia afya njema ni familia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius
Nyerere ambayo imeeleza kupokea kwa masikitiko taarifa za kuugua kwake
na kumwombea apone haraka ili aendelee na majukumu yake kwa Taifa.
Chama cha RPP cha Rwanda kimemtumia salamu za pole
Rais Kikwete na kuungana na mamilioni ya Watanzania kumwombea ili
arejee katika afya yake na majukumu ya kila siku. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz