Wanaharakati
watatu wa kisiasa nchini Libya wamechinjwa baada ya kuandika katika
mitandao ya kijamii juu ya maisha chini ya utawala wa dola ya
kiislam.Miili yao ilipatikana mapema wiki hii mashariki mwa mji wa Derna
karibu na Benghazi.
Tukio hilo lilianzia kwa wanaharakati hao
kutekwa mapema mwezi huu.Mji huo wa Derna uko chini ya mamlaka ya
kikundi cha dola ya kiislam tangu mwaka 2012 ambacho kimekiri kuwa
sehemu ya kundi la is.Mnamo mwezi August mwaka huu katika video ilooneshwa katika mitandao ya kijamii ilionesha mwanamume mmoja akipigwa risasi na kufa hadharani katika viwanja vya mpira mjini Derna.
Siku za hivi karibuni kuna picha iloachiliwa mitandaoni ikionesha kikundi cha kijamii kinachojiita mahakama ya kiislam. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na BBC Swahili
No comments:
Post a Comment