Askofu Kiongozi wa
Kanisa la Moravian Tanzania, Alinikisa Cheyo amezuiwa na waumini wa
kanisa hilo kuingia katika ofisi yake iliyopo Jakaranda, Mbeya kwa saa
18.
Cheyo, ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la
Moravian Jimbo la Kusini Magharibi, alifungiwa mlango na waumini wa
kanisa hilo Usharika wa Jakaranda kumzuia asiingie mpaka atakapoitisha
mkutano na kumrudisha Mchungaji Nosigwe Buya ambaye alimhamisha.
Akizungumzia hatua hiyo mbele ya waumini wengine,
Mchungaji wa usharika huo, Jamson Mwilugumo alisema walifunga mlango huo
kushinikiza Askofu Cheyo abadili msimamo wa kumwondoa Mchungaji Buya na
kumrejeshea wadhifa wake wa Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya jimbo
hilo. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Jitihada za Askofu Cheyo kuwasihi waumini hao
kufungua milango iliyokuwa imefungwa kwa minyororo hazikufua dafu hadi
alipoomba msaada wa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk Norman Sigala.
Baada ya kufika katika eneo hilo, Dk Sigala ambaye
aliambatana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi aliwataka
waumini hao wafungue mlango huo na kutoa maelekezo kwa Askofu Cheyo
kuhakikisha kuwa anaitisha mkutano wa Halmashauri Novemba 15, mwaka huu
bila kukosa ili kumaliza mgogoro huo.
Kauli hiyo ilipokewa kwa furaha na waumini hao ambao walifungua mlango.
Akizungumza mbele ya Dk Sigala, Askofu Cheyo
alikubali kuitisha mkutano kumaliza mgogoro huo kama kiongozi huyo wa
Serikali alivyoelekeza.
Mgogoro ulikoanzia
Mgogoro huo ulianza Aprili 30, mwaka huu katika
mkutano wa Halmashauri hasa katika suala la ujenzi wa Shule ya Sekondari
ya Mbozi. Ilidaiwa kuwa katika kikao hicho, Askofu Cheyo aliamuru Buya
na makamu wake watoke nje ya kikao na kufanya uchaguzi mpya na kumchagua
mwenyekiti.
Mgogoro huo uliibuka tena Julai 15, mwaka huu
wakati waumini hao walipofunga ofisi hizo kwa zaidi ya saa tano
wakishinikiza kuitishwa mkutano wa halmashauri ya usharika huo.
Katika mgogoro huo, Askofu Cheyo amekuwa akisema kwamba unatokana na baadhi ya watu wenye uroho wa madaraka. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment