Mgombea wa urais
kupitia tiketi ya chama cha Republican Marco Rubio amemshtumu Donald
Trump kwa kusema kuwa Uislamu unachukia Marekani katika mjadala uliokuwa
moja kwa moja runingani.
Bwana Rubio ambaye anakabiliwa na
ushindani wa maisha yake katika jimbo la Florida siku ya Jumanne amesema
kuwa Uislamu una tatizo la itikadi kali lakini akaongezea kuwa Waislamu
wengi wanapenda Wamerekani.
''Marais hawawezi kusema kile wanachotaka ,kuna madhara'',alisema huku raia wakimpigia makofi. Wagombea hao wanne wa chama cha Republican walisikia maombi kutoka kwa viongozi wa chama hicho kuwa na mjadala wa amani.
Ikilinganishwa
na mjadala uliopita ambao ulikabiliwa na na matusi ya kibinafsi mjadala
huu ulikuwa na muongozo mzuri huku wagombea wote wakitoa malengo ya
sera zao.
''Kufikia sasa siamini vile tumekuwa watulivu hapa'',bwana Trump alinukuliwa akisema. Lakini
katika swala la Uislamu,kulikuwa na tofauti kubwa kati ya Trump na
wagombea wengine huku wenzake wote wakitofautiana naye kwamba familia za
magaidi ziangamizwe. Like page yetu ya facebook Jambo Tz
No comments:
Post a Comment