MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amevunja ukimya na kusema atawasilisha jina makini la mrithi wa nafasi ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa.
Akizungumza mjini hapa jana, baada ya kumalizika kikao cha kwanza cha Kamati Kuu, Mbowe alisema sifa za kiongozi anayepaswa kushika wadhifa huo zinafahamika.
Alisema wajumbe na wanachama wa Chadema watarajie kumpokea mtu makini ambaye jina lake atalipendekeza kisha kupigiwa kura na wajumbe wa Baraza Kuu kesho. Like page yetu ya facebook Jambo Tz
“Sifa za Katibu Mkuu zinajulikana, nawaomba
wanachama na wajumbe kutulia, jina watakutana nalo ukumbuni muda ukifika… nina
imani litakuwa jina la mtu makini,” alisema.
Mbowe alisema chama hicho kinakutana kwa mara
ya kwanza tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa Rais mwaka jana, hivyo wana
mambo mengi ya kujadili, ikiwa ni pamoja na kupanga mikakati mipya ya kuwafikia
wafuasi wao.
Katika hatua nyingine, chama hicho kimesema
kitamtambulisha Katibu Mkuu mpya rasmi Jumapili wakati wa mkutano wa hadhara
utakaofanyika viwanja wa Furahisha jijini hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana,
Ofisa Habari wa chama hicho, Tumaini Makene, alisema majina mawili
yatawasilishwa katika Baraza Kuu litakalokaa usiku wa Jumamosi kwa ajili ya
kupitisha jina moja.
Alisema majina yatakayowasilishwa hayatakuwa
na uhusiano au urafiki wowote na Mwenyekiti Mbowe.
“Tayari
viongozi wa kitaifa wamewasili Mwanza, Sekretarieti imekutana kwa ajili ya
kuandaa ajenda ambazo zitajadiliwa na Kamati Kuu yenye wajumbe 36.
“Siku
inayofuata Baraza Kuu litakaa usiku kwa ajili kumpata Katibu Mkuu, hii ni
nafasi nyeti sana ndiyo maana hata wenzetu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
wanafuatilia kwa ukaribu kujua nani atapewa mikoba ya Dk. Willibrod Slaa. Like
page yetu ya facebook Jambo Tz
No comments:
Post a Comment