Imeelezwa kuwa
maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU), yanaweza kuongezeka nchini hasa
kwa vijana kutokana na kubainika kupungua kwa kasi ya matumizi ya mipira
(kondomu).
Hayo yalielezwa jana na Katibu Mkuu, Ofisi ya
Waziri Mkuu, Dk Florens Turuka katika mkutano wa sita wa kutathmini
maambukizi ya VVU nchini.
Dk Turuka alisema maambukizi mapya yameendelea kuwapo kwa sababu vijana hawatumii kondomu kujikinga.
“Matumizi ya kondomu katika jamii yamepungua na
kuwafanya watu wengi hasa vijana kupata maambukizi na zaidi ni kutokana
na mwamko mdogo kuhusu umuhimu wa kondomu kama kinga ya Ukimwi,”
alisema. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Alisema utafiti uliofanyika mwaka jana ulionyesha
kuwa asilimia 50 ya waliojitokeza kupima VVU na kupata ushauri, walikiri
kutotumia kondomu. Hata hivyo, Dk Turuka alisema katika kipindi cha
miaka 10 iliyopita, maambukizi mapya yalipungua kutoka watu 180,000 hadi
72,000 kwa mwaka.
Alisema licha ya kuwapo mafanikio hayo, kiwango
cha matumizi ya kondomu kimeshuka na kuhatarisha maisha ya vijana wenye
umri kati ya miaka 15 – 39.
Alisema mwaka ujao wa fedha, Serikali itaanzisha
mfuko maalumu wa kukusanya fedha kwa ajili ya kununulia dawa za
kupunguza makali ya ugonjwa huo (ARV).
Alisema zaidi ya nusu ya wagonjwa walioathirika wanahitaji dawa hizo.
Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti
Ukimwi (Tacaids), Fatma Mrisho alisema wanafanya jitihada kuhakikisha
wanapunguza maambukizi mapya hadi kufikia sifuri ifikapo mwaka 2020.
Aliitaja baadhi ya mikoa yenye idadi kubwa ya maambukizi mapya kuwa ni Njombe, Shinyanga, Mbeya, Dar es Salaam na Ruvuma.
“Katika miaka miwili ijayo, tutaelekeza nguvu zetu
kwenye mambo yanayochangia kuongezeka kwa maambukizi mapya, ikiwamo
maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na kukabiliana na uhaba wa
dawa,” alisema. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment