Mjadala kuhusu masuala ya Muungano unatarajiwa kurejea upya katika kamati za Bunge Maalumu leo, wakati zitakapoanza kujadili sura za saba, nane, kumi na moja, 18 na 15 za Rasimu ya Katiba.
Kamati zimepewa siku sita kujadili sura hizo tano
ambazo zina jumla ya ibara 79, huku miongoni mwake zikigusa masuala
mengi ambayo msingi wake umejengwa juu ya mfumo wa serikali tatu.
Miongoni mwa masuala hayo ni pamoja na baraza la
mawaziri, tume ya kusimamia na kuratibu uhusiano baina ya Serikali ya
Muungano na Serikali za Nchi Washirika (Tanganyika na Zanzibar),
Sekretarieti ya Tume ya Uhusiano na Uratibu, Masuala yanayohusu Benki
Kuu na Fedha pamoja na uteuzi wa watumishi katika Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Suala la aina ya muungano lilianza kujadiliwa
katika sura ya kwanza na ya sita katika awamu ya kwanza ya Bunge
iliyomalizika mwishoni mwa Aprili mwaka huu na kuzua mvutano mkali ambao
hatimaye ulisababisha baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu kususia
mchakato huo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz