Katibu
Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu akiongea na waandishi wa habari
leo makao makuu ya klabu ya Yanga, kushoto kwake ni Kocha Mkuu Marcio
Maximo na afisa habari Baraka Kizuguto
Uongozi wa klabu ya Young
Africans leo umefanya mkutano na waandishi wa habari juu na kusema
kilichofanywa na waandaji wa michuano ya Kombe la Vilabu Bingwa ukanda
wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuiondoa timu isishiriki ni cha
kushangaza sana na kinadidimiza soka kwa ujumla.
Katibu Mkuu wa Young Africans Bw
Beno Njovu amesema walipata barua ya mwaliko wa kushiriki mashindano
tarehe 25/7/2014 na kudhibitisha kushiriki michuano hiyo kwa kuandika
barua iliyokwenda TFF na kisha wao kuiwasilisha kwa CECAFA.
“Baada ya kudhibitisha kushiriki
michuano hiyo tuliambiwa na CECAFA tutume orodha ya wachezaji na
viongozi ambao watasafiri kuelekea nchini Rwanda kwenye michuano hiyo
ili waweze kuandaa tiketi za ndege na sehemu ya malazi kitu ambacho
tulitimiza” alisema Beno.
Lakini katika hali ya kushangaza
jana tulipokea barua kutoka TFF ikisema CECAFA imetuondoa kwenye
mashindano hayo kwa kushindwa kukidhi vigezo na kuiteua timu ya Azam
kuchukua nafasi yetu “aliongeza Beno.”