Katibu
Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu akiongea na waandishi wa habari
leo makao makuu ya klabu ya Yanga, kushoto kwake ni Kocha Mkuu Marcio
Maximo na afisa habari Baraka Kizuguto
Uongozi wa klabu ya Young
Africans leo umefanya mkutano na waandishi wa habari juu na kusema
kilichofanywa na waandaji wa michuano ya Kombe la Vilabu Bingwa ukanda
wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuiondoa timu isishiriki ni cha
kushangaza sana na kinadidimiza soka kwa ujumla.
Katibu Mkuu wa Young Africans Bw
Beno Njovu amesema walipata barua ya mwaliko wa kushiriki mashindano
tarehe 25/7/2014 na kudhibitisha kushiriki michuano hiyo kwa kuandika
barua iliyokwenda TFF na kisha wao kuiwasilisha kwa CECAFA.
“Baada ya kudhibitisha kushiriki
michuano hiyo tuliambiwa na CECAFA tutume orodha ya wachezaji na
viongozi ambao watasafiri kuelekea nchini Rwanda kwenye michuano hiyo
ili waweze kuandaa tiketi za ndege na sehemu ya malazi kitu ambacho
tulitimiza” alisema Beno.
Lakini katika hali ya kushangaza
jana tulipokea barua kutoka TFF ikisema CECAFA imetuondoa kwenye
mashindano hayo kwa kushindwa kukidhi vigezo na kuiteua timu ya Azam
kuchukua nafasi yetu “aliongeza Beno.”
Kanuni za CECAFA zipo wazi kuwa
wachezaji wanaopaswa kushiriki michuano hiyo ni lazima wawe na leseni za
kucheza mpira kutoka kwa chama husika, jambo ambalo ambalo orodha
tuliyowapelekea wachezaji wote wataichezea Yanga msimu huu wa 2014/2015.
Kocha Marcio Maximo alianza
maandalizi ya kikosi ambacho kingekwenda kushiriki michuano hiyo ambayo
ilipaswa kuanza ijumaa tarehe 8/8/2014 kwa Yanga kufungua dimba la
wenyeji timu ya Rayon FC .
Kikosi ambacho kocha mkuu
alikichagua kwenda kwenye michuano ya Kagame kilikua na jumla ya
wachezaji 20, 15 wakiwa kutoka timu ya kikosi cha wakubwa na wachezaji
watano wakitoka kikosi cha pili U20 chini ya kocha Leonado Neiva ambaye
amekua na wachezaji hao kwa takribani mwezi mmoja.
Lakini walichokiamua CECAFA ni
kuiondoa klabu ya Yanga na kuipa nafasi timu nyingine kwa kusema kikosi
kilichopelekwa hawakubaliani nacho na hata kocha mkuu Marcio Maximo
haendi, hao ndo tulipojua ya kuwa wanataka majina ya watu na sio timu.
Zifuatazo ni sababu za Kiufundi ambazo Yanga ilizipelekea CECAFA kuhusu kikosi hicho kutojumuisha wachezaji wa timu za Taifa.
a) Ripoti ya kocha aliyeondoka Yanga msimu uliopita Hans
ilitoa maelekezo ya kupunguza wachezaji tisa (9) na wachezaji wawili
kujiunga na klabu ya Azam hivyo kufanya kikosi kupungua wachezaji 11
kutoka katika idadi ya wachezaji 30 wa msimu uliopita. b)
Wachezaji 10 wa Yanga wamekuwa na majukumu ya timu za Taifa za Tanzania
(Taifa Stars), Rwanda na Uganda tangu Aprili 19, 2014 mpaka mwanzoni
mwa Agosti, takribani miezi mitatu wamekuwa kambini bila kupata muda wa
kupumzika. c) Benchi la Ufundi la Yanga ni jipya
kuanzia kocha mkuu Maximo na wasaidizi wake watatu Leonardo Neiva,
Salavatory Edwarda na Shadrack Nsajigwa hivyo wanahitaji muda wa kuwajua
wachezaji waliokuwa kwenye timu ya Taifa ndo maana hawakuwajumuisha
kwenye kikosi cha kwenda Kigali Rwanda. d) Baadhi ya
wachezaji wanahitaji Vibali vya kufanyia kazi nchini, uhamisho wa
Kimataifa (ITC) ili waweza kushiriki michuano ya Kagame, na moja ya
kanuni za CECAFA mchezaji anayeshiriki mashindano hayo ni lazima awe na
leseni ya kucheza mpira kwa ligi ya ndani. e) Katika
wachezaji 20 waliochaguliwa kushiriki michuano ya Kagame, wachezaji 6
wamepandishwa moja moja katika kikosi cha wakubwa msimu huu hivyo
kufanya idadi ya wachezaji wa U20 kuwa watano tu. f)
Wachezaji walikokuwa kambini Taifa Stars kwa takribani miezi mitatu bila
ya kupumzika, daktari alipendekeza wapate japo siku kumi na nne (14) za
kupumzika ili miili yao iweze kupoa na kuanza upya tena maandalizi ya
msimu mpya. g) Yangga tunaamini hakuna mtu yoyote zaidi
ya Kocha Mkuu anayeweza kutupangia kikosi cha kwanza, sababu yeye ndio
anayekaa na wachezaji mda wote na kujua ubora wa wachezaji wake. Chanzo: Tovuti ya Yanga sc
No comments:
Post a Comment